Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

10. Paka
Watu wengi hufikiri ya kwamba paka ni mnyama ambaye anafugwa kwa lengo la kufukuza panya, ingawa panya huogopa paka lakini si jukumu la paka kuwinda panya ndio afanye mlo, paka ni mnyama kwa ajili ya urembo tuu, akiwa na afya nzuri akanawiri huwa na kazi ya kupendezesha nyumba yako, hivyo usimnyime chakula kwa kusema atakuwa mzembe kukamata panya.
 
Mbuzi.
Ondolea mbali kwamba ni mnyama mdogo lakini nyama yake huuzwa ghari zaidi kuliko nyama zingine zote ambazo upatikanaji wake ni rahisi, pia ni miongoni mwa viumbe ambavyo nyama yake huuzwa sana nje ya nchi, mbali na faida hizo mnyama huyu hutoa maziwa, pia ngozi yake huingizwa katika biashara.
 
Kuku
Pamoja kwamba ni moja ya mifugo ambayo ni pasua kichwa sana, lakini unapofanikiwa kuiweka katika mstari mnyofu kuku huwa na faida sana, kwanza ni zao la biashara katika suala la mayai yake, ni chanzo cha mapato kwakuwa soko lake ni kubwa na pia kuku wenyewe ni waweza kuwa chakula kwa mfugaji.
 
6.punda
Pengine ukiwekewa mbuzi na punda waweza mpa daraja kubwa mbuzi, lakini kama utazingatia faida zao utaweza gundua ya kwamba punda ndiye mwenye faida zaidi, mosi punda nyama yake hutumika kama kitoweo, maziwa yake pia chakula, ni mnyama ambaye anaheshimika kwa kubeba mizigo mizito, ni usafiri na ngozi yake hutumika kwa biashara pia kwato.
 
N'gombe
Nyama ya kiumbe huyu yawezekana kabisa ndio ikawa nyama maarufu sana kutokana na upatikanaji wake wa urahisi wa bei na uwingi wake, pia ni kiumbe ambaye nyama yake yatumiwa karibu na makabila yote, pia dini zote kwa hapa Afrika, faida zake ni nyingi mnoo pamoja kwamba ndiye mnyama ambaye nyama yake ndio chakula kikuu, lakini pia ni mnyama wa biashara katika ngozi, kwato,pembe pamoja na mifupa yake, ni cha mapato katika ngazi ya familia hususani uuzaji wa maziwa yake, ng'ombe pia hutumiwa katika kilimo na huko Thailand ndio kabisa viumbe hawa hutumika kusafirisha abiria kabisa.
 
Mbwa.
Faida yake yaweza isionekane kirahisi hasa kwa kuzingatia aina ya matunzo tunayowapa huku kwetu uswahilini, lakini mbwa ni viumbe ambao wanafaida kubwa iwapo watakuwa na matunzo mazuri, mbali na kuwa mnyama ambaye biashara yake inafanya vyema, pia viumbe hawa hutumiwa katika michezo ya mashindano mbalimbali ambayo huwa chanzo cha mapato kwa watu, mbwa pia yafahamika wazi kuwa ni ulinzi thabiti, huwasaidia polisi kutawanya maandamano, na kubwa kuliko yote ambalo pengine nchi zetu huku halijafika ni kwamba mbwa hutumika kuwaongoza watu wenye ulemavu wa macho katika shughuli zao za kila siku.
 
Kondoo.
Ni mnyama mpole ambaye anaonekana hana makuu, hapendi kiki na aliyoipenda haikumtoa vilivyo ingawaje wakifanya wengine lingekuwa gumzo, ni mnyama mwenye ujasiri wa kupambana na radi, nyama yake upatikanaji wake si mwepesi na pengine hata wakisema ifantike sensa ya wangapi ambao wameshakula nyama yake majibu yatakuwa dhaifu, ufugaji wa mnyama huyu umekuwa haba sana na haupewi nafasi kabisa na serikali sijui kwanini ? Ni mnyama ambaye ana faida lukuki sana na nzito, sina mashaka hii ya utoaji wa maziwa na nyama zaweza kuwa za mashaka, ufugaji wa kondoo pia ni mzuri kwa biashara kwani vinyweleo vyao husaidia upatikanaji wa sufi, na faida ya sufi yafahamika, ngozi yake pia ni biashara lakini kubwa kuliko yote ni kwamba mnyama huyu yawezekana kabisa akawa na msaada kwa wagonjwa wa kisukari, kwani kongosho yake inavimelea vya kutosha vya kupambana na maradhi hayo.
 
2.ngamia.
Ni wazi wanyama hawa wenye faida kubwa duniani ndio ufugaji wao ni dhaifu kabisa, maziwa ya ngamia mbali ya kuwa ni ghari kuliko maziwa yoyote, lakini ni chakula ambacho ndani yake kimebeba matibabu ya asili, ngamia ni usafiri, ni utalii, ni biashara, ni chakula.
 
1.Farasi.
Farasi ndio mnyama pekee ambaye anabeba sifa karibia za wanyama wenzie wote, kwanza nyama yake ni chakula kama ilivyo kwa wanyama wengine, maziwa yake ni chakula kama wanyama wengine, ni mnyama ambaye hutumika kama usafiri na tena wa haraka kuliko wote, kwenye ulinzi pia yupo kama alivyo mbwa, na yeye hutumiwa kutawanya maandamano, Kama ilivyo kwa kondoo na yeye sampuli ya damu yake imetumika sana kutengeneza dawa za aleji, anatumiwa katika kilimo pia, mizigo anabeba, ni mnyama wa biashara mnaoendaga 77 na 88, najua mshapanda sana kwa 3000, ni mnyama anayemuepusha boss wake na hatari, ni mnyama ambaye anauzwa ghari kuliko wanyama wengine hapo juu na mengine mengi anayo.
Kufikia hapo najua ukitaka kufuga utazingatia mambo mengi sana, basi kama ni hivyo nikutakie mafanikio mema.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…