Manchester United itawakosa nyota wake David de Gea na Paul Pogba katika mchezo wao muhimu dhidi ya Liverpool utakaochezwa Jumapili kwenye Uwanja Old Trafford.
Kipa huyo anatakiwa kufanyiwa vipimo na madaktari wa timu yake wakati atakaporejea Carrington leo Alhamisi, lakini kocha Ole Gunnar Solskjaer amekiri jana usiku kuwa haoni kama ataweza kucheza mechi hiyo.