JUMATATU iliyopita, Cristiano Ronaldo alifikisha bao lake la 700 katika maisha yake ya soka, wakati alipofunga mara moja akiwa na Ureno kwenye mechi ya kipigo kutoka kwa Ukraine kwenye mikikimikiki ya kuwania Euro 2020.
Ronaldo alifunga mabao matano katika mechi 31 alizochezea Sporting CP, mabao 118 katika mechi 292 alizoichezea Manchester United, mabao 451 katika mechi 438 alizocheza kwenye kikosi cha Real Madrid na mabao 32 amefunga kwenye mechi 51 alizochezea klabu yake ya sasa ya Juventus.
Mabao mengine alifunga akiwa na kikosi cha timu ya taifa ya Ureno na hivyo kuingia kwenye kundi la mastaa wachache sana kwenye dunia ya soka waliofikisha mabao 700 katika maisha yao ya soka.
Gwiji huyo alifunga pia bao la ushindi wakati Ujerumani Magharibu wanabeba Kombe la Dunia 1974, huku akiwa na wastaani balaa wa mabao, ambapo kwenye timu ya taifa, amefunga mabao 68 katika mechi 62.
Wakati akiaminika kuwa mmoja wa wanasoka bora wa muda wote, Puskas, aliyekuwa akifahamika kama ‘Galloping Major’ alitamba na kmikosi cha Hungary na Real Madrid, aliyotamba nayo kwenye michuano kibao ikiwamo ya Kombe la Ulaya mwaka 1960.