Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Umahiri wake wa kufunga mabao makali, yanamfanya jina lake litumike kwenye ile tuzo ya Bao Bora la Mwaka inayotolewa na Fifa, ‘The FIFA Puskas Award’, ambapo imekuwa ikitolewa kila mwaka kwa mchezaji anayefunga bao bora zaidi kwa mwaka husika.
 
Pele (mabao 767)

Mbrazili Pele bado anatambulika kama mmoja wa watu waliohamasisha zaidi soka duniani, huku akiingia kwenye kitabu cha rekodi cha Guiness cha kufunga mabao mengi kwa mechi, baada ya kudaiwa amefunga mabao 1281 katika mechi 1363.
 
Mshindi huyo mara tatu wa Kombe la Dunia akiwa na Brazili, Mfalme Pele alifunga mabao 767 katika mechi 831 na hivyo kuwa na wastani mzuri wa kufikisha idadi ya mabao 700 na kuendelea ndani ya mechi chache. Bao lake la kichwa alilofunga kwenye Kombe la Dunia 1970 lilikuwa la 100 kwa Brazil.
 
Romario (mabao 772)

Akiwa na mabao 772 katika mechi 994, Romario anatajwa kama mchezaji hodari zaidi kwa kufunga kuwahi kutokea duniani. Kwa sasa akifanya kazi ya siasa huko kwao Brazil, Romario alitajwa kuwa Mchezaji Bora wa Dunia mwaka 1994 na alikuwa sambamba na Pele, alipochaguliwa na raia kwenye timu ya Fifa ya mwaka 2002.
 
Akijitengenezea umaarufu wa kuwa mchezaji aliyetumia vizuri zaidi miguu yote miwili, Bican alicheza klabu kadhaa huko kwao Austria kabla ya kwenda kukipiga kwenye timu nyingine kadhaa Jamhuri ya Czech, ikiwamo Dynamo Prague. Alicheza pia Bohemia na Moravia.
 
73106560_166431857878199_8023284792535094130_n.jpg
 
Back
Top Bottom