Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Farasi ni mnyama mwenye nidhamu sana. Ukimpanda, halafu ukaanguka, hawezi kuendelea na safari mpaka utapozinduka, hata kama ulizimia. Pia, farasi ni mnyama mwenye upendo kiasi kwamba hawezi kukupeleka sehemu yenye hatari. Ukiona anagoma kusonga mbele, tambua kuwa aidha kuna nyoka au hatari nyingine usiyoweza kuiona.
 
Macho ya farasi ni makubwa sana na yana uwezo mzuri wa kunasa matukio vyema, mbele na nyuma, na kwa umakini. Mbali na uwezo huo wa kuona vyema lakini pia farasi yupo vizuri katika kunusa. Ukiwa na farasi, hamuwezi kukamatwa kirahisi na wanyama wakali hasa wale wanaovizia kwa kujificha.
 
Farasi hula kilo tano mpaka 12 za majani kwa siku, hutegemeana na umri pamoja na uzito wake. Wanyama pekee wanaokula nyama wanaoyeweza kumkamata kwa kumfukuza ni duma na mbwa mwitu wa kizungu (wolf). Hawa wengine akina simba, fisi – nyama yake wataishia kuisikia tuu
 
Mbali na uwezo huo wa kuchanja mbuga, farasi pia hupatwa na hisia na maumivu. Ukimtendea ubaya, usichangae akidondosha machozi na akikushusha kuanzia juu mpaka chini. Hapo ujue amekudharau tuu. Wanyama hawa huuzwa ghali sana. Farasi mmoja kwa hapa kwetu hufikia hadi milioni tano na ushee.
 
Bei ya farasi hupangwa kutokana na rangi, siyo ukubwa. Rangi adimu ndiyo huwa ghali zaidi. Hivyo basi, nyeupe na nyeusi si rangi ghali katika kumnunua farasi, labda ziwe na mngaro wa kipekee. Allah amejaalia umri wa kuishi farasi, wakipata matunzo mazuri, hufikia hadi miaka kati ya 28 hadi 32.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…