Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Vyakula mbalimbali ambavyo watu wanaweza kuandaa kutokana na zao la muhogo ni pamoja na:
Mkate ambao unaweza kuandaliwa kutokana na unga wa mhogo pekee au mchganyiko wa unga wa muhogo na ngano
Vibanzi
Chips
Mkate wa muhogo uliookwa katika tui la nazi
Keki ya muhogo
Muhogo uliopikwa katika mchuzi wa nazi
 
Keki ya muhogo natamani nijue kupika.
 
Pamoja na kuliwa na watu katika namna mbalimbali, zao hili pia hutumika kutengeneza unga wa muhogo unaoliwa kama ugali nchini Tanzania, kuandaa wanga ambao hutumika viwandani, kulishia Wanyama, na kutengeneza madawa, nguo, karatasi, na vifaa vya ujenzi.
 
Faida za kula muhogo na unga wa muhogo a.k.a udaga
Muhogo una karibu mara mbili ya kiwango cha kalori kuliko inayopatikana katika viazi. Ni moja ya chakula chenye kalori nyingi zaidi kuliko mazao mengine ya mizizi na majani yanayopatikana katika ukanda wa Kitropiki. Ukila gramu 100 za muhogo unakuwa umeingiza katika mwili wako kalori 160. Hii ni kwa sababu kiwango hiki kikubwa cha kalori hutokana na sukari aina ya sucrose ambayo ni asilimia 69 ya Jumla ya sukari inayopatikana katika chakula hiki.
 
Pamoja na kwamba muhogo una protini na mafuta kwa kiasi kidogo kuliko mazao ya nafaka, bado kiwang hiki ni kikubwa kuliko kile kinachopatikana katika mazao mengine ya mizizi kama vile viazi na magimbi. Hivyo kula muhogo kwa wingi!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…