Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Mtu akikuita mjinga au mpumbavu juu ya maisha yako usikasirike kwa sababu wewe si mjinga wala mpumbavu. Sema hapana kwa ndiyo nyingi kwa sababu hawapaswi kuingilia mambo ya mtu mwingine bila idhini ya Mwenyezi Mungu. Kuingilia mambo ya mtu mwingine bila idhini ya Mwenyezi Mungu ni dhambi, tena dhambi kubwa, ni kuvunja amri kuu ya kwanza ya Mungu.
 
Usiingilie mambo ya mtu mwingine bila kibali kutoka kwa Mungu. Kuingilia mambo ya mtu mwingine bila kibali kutoka kwa Mungu ni dhambi. Dhambi hiyo itakuathiri. Hivyo, jali mambo yako – ya mwingine Mungu anayafanyia kazi – hadi utakapoitwa na Mungu kuingilia kati. Kuingilia kati mambo ya mtu mwingine kunaweza kuathiri mpango wa Mungu katika maisha yake. Hivyo, acha.
 
Mtu akikuita mjinga au mpumbavu juu ya maisha yako usikasirike kwa sababu wewe si mjinga wala mpumbavu. Sema hapana kwa ndiyo nyingi kwa sababu hawapaswi kuingilia mambo ya mtu mwingine bila idhini ya Mwenyezi Mungu. Kuingilia mambo ya mtu mwingine bila idhini ya Mwenyezi Mungu ni dhambi, tena dhambi kubwa, ni kuvunja amri kuu ya kwanza ya Mungu.
Hehe na wewe usituingilie wabara na sembe letu
 
Kama John Doe ana matatizo katika maisha yake acha ayatatue mwenyewe. Akishindwa atakuomba ushauri au ataomba ushauri kutoka kanisani kama ni Mkristo, au msikitini kama Mwislamu, au kutoka katika nyumba yoyote ya ibada kulingana na imani yake. Mtu akikuomba ushauri mshauri kwa moyo wako wote, wala usimshauri kwa unafiki au kinyongo cha aina yoyote ile.
 
Wewe kuingilia mambo ya John ni sawa na kusema, “Mungu umeshindwa hebu ngoja na mimi nijaribu; ngoja niingilie kati kukusaidia juu ya maisha ya John Doe.” Hiyo ni dhambi. Tena ni dhambi kubwa. Unajifananisha na Mungu; kwamba Mungu wa John Doe ameshindwa kwa hiyo mungu wewe ndiye utakayemtatulia matatizo yake.
 
Amri kuu ya kwanza ya Mungu inasema, “Usiwe na miungu mingine ila mimi.” Kuingilia mambo ya John tayari umevunja amri ya kwanza ya Mungu kwa kujifanya Mungu. Mungu ana mpango na maisha ya John, na anatumia matatizo yake kumfikisha kwenye takdiri aliyompangia. Hivyo, wewe si Mungu, acha Mungu afanye kazi yake
 
255625562879_status_c88445ef7a654be3a46417cd47c1ee10.jpg
Daemusin
 
Kuna kitu kibaya sana ndani ya mtu. Hilo liko wazi. Biblia inasema chanzo cha matatizo ya mtu ni moyo wake, roho yake, pamoja na uwezo wake wa kufikiri. Tumejaa ulaghai, unafiki na utata. Tunajichezea sisi wenyewe ule mchezo wa kitoto wa kombolela. Yaani, tunajificha na kujitafuta wenyewe, tunawadanganya watu lakini Mungu anatuona.
 
Labda ni katika mazingira hayo ambapo moyo hufanya kazi yake kwa uharibifu zaidi. Huficha uovu mkubwa wa dhambi unaoendelea kuwa mkubwa, na matokeo yake kuwa mabaya na mazito zaidi. Moyo unatulaghai katika kufikiri kuwa si mbaya, au kwamba Mungu ni mwenye huruma sana kiasi kwamba atapuuza.
 
Tusipoacha kutenda dhambi, dhambi haitakomeshwa. Ni wajibu wa kila mmoja wetu kukomesha dhambi katika maisha yake. Usisubiri wengine waikomeshe kabla au kwa niaba yako. Hata serikali haitaweza kukusaidia.

Kuna namna moja tu ya kukomesha dhambi, nayo ni kufunga milango yote ya dhambi baada ya kumkaribisha Mungu katika maisha yako.

Funga milango yako yote ya dhambi na kaa mbali na nyavu zinazowinda watu kabla miguu yako haijanaswa na nyavu hizo.
 
Mungu akikubariki kipaji chako watu watasema ni laana. Maisha yako ni sawa na mto. Unakoelekea ni baharini. Lakini sasa umefika kwenye mlango wa bahari. Unahangaika upite wapi kufika baharini, ambapo utaogelea kwa kadiri utakavyoweza. Utakapofika baharini, watu, badala ya kusema umebarikiwa, watasema umelaaniwa, badala ya kukuita malaika, watakuita shetani.
 
Back
Top Bottom