Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Usioshe matunda au mboga mboga kabla ya kuzihifadhi
Ajabu sivyo?
Kwamba usioshe matunda kabla ya kuhifadhi kwenye jokofu au kabatini?
Ndiyo.
Ni bora kutoyaosha kabisa kabla ya kuhifadhi. Kwa nini? kwa sababu kuosha huondoa baadhi ya ulinzi wa asili wa vyakula hivi na kusababisha kuoza au kupata uvundo kwa haraka zaidi.
Badala yake tumia tishu au kitambaa safi kupangusa vumbi na uchafu kisha hifadhi. Osha kabla ya kula.
 
Tunza matunda na mbogamboga mahali pakavu
Unapoweka matunda na mboga mboga kwenye jokofu au sehemu yenye unyevu unakuwa unakaribisha uvundo.
Fanya hivi kama unataka matunda na mboga mboga kukaa kwa muda mrefu:
Pangusa matunda kwa kitambaa au tishu
Chukua kifaa kikavu cha kutunza (kwa mfano chombo cha plastiki)
Tanguliza kitambaa safi katika chombo hicho kisha weka matunda au mboga mboga)
Funika kuhakikisha matunda au mboga mboga hazionekani
Weka chombo hicho kwenye jokofu au kabati lililo wazi kuruhusu hewa kuzunguka.
 
Tunza parachichi kwenye mfuko au gazeti
Unajua njia nzuri ya kuivisha na kutunza parahichi?
Ni rahisi sana. Fanya hivi:
Safisha parachichi bichi (mara nyingi tunanunua mabichi kiasi) kwa kitambaa au tishu
Liweke kwenye mfuko wa plastiki (paper bag) au kipande cha gazeti.
Liweke mahali pakavu (kwenye kabati kwa mfano) mpaka liive
Baada ya kuiva liweke kwenye kitambaa safi ndani ya chombo kikavu kisha tunza kwenye jokofu
Kutunza parahichi kwa namna hii kutakusaidia kuongeza muda wa kudumu hasa kama umeyanunua mengi kwa ajili ya familia.
 
Si kila matunda au mboga mboga hutunzwa kwenye jokofu
Wengi hatujui. Hata mimi sikuwa najua hili.
Si kila chakula (hasa matunda na mboga mboga) hufaa kutunzwa ndani ya jokofu.
Kwa mfano matunda kama vile pilipili, matango, na nyanya hayapaswi kuhifadhiwa ndani ya jokofu. Na kama u mzoefu wa hili utagundua kuwa vyakula hivi huwa na ladha tofauti na mara nyingi husinyaa.
Tunza vyakula hivi mahali pakavu ndani ya kitambaa safi.
 
Kwa mfano ndizi mbivu hubadilika rangi na kuwa nyeusi huku ngozi ikibadilika na kuwa laini sana inapotunzwa kwenye jokofu. Kama unataka ndizi mbivu zikae muda mrefu fanya hivi:
Chukua mfuko wa plastiki na ufunge kwa kamba katika kikonyo cha ndizi
Ziweke ndizi hizo kwenye kitambaa safi ndani ya chombo.
Tunza kwenye kabati mahali ambako kuna jotoridi la kawaida (room temperature)
 
Tunza baadhi ya mbogamboga ndani ya maji
Mgoga mboga kama vile karoti na figili huweza kudumu kwa muda mrefu kama zitatunzwa ndani ya maji.
Unachopaswa kufanya ni kukatakata mboga hizi katika vipande kisha kuviweka katika chombo chenye maji kiasi.
Weka chombo hicho ndani ya jokofu
 
Usiweke matunda na mboga mboga sehemu ya ‘freezer’ katika jokofu
Matunda na mboga mboga hayapaswi kutunzwa sehemu zenye baridi kali katika jokofu. Kadri joto linavyokuwa dogo sana ndivyo vyakula hivi vinavyopoteza uhalisi wa harufu na ladha.
Kama unataka vyakula hivi kudumu kwa muda mrefu na kubaki na ladha nzuri, hakikisha unavitunza katika sehemu za jokofu kuliko na joto la kawaida.
 
Baadhi ya matunda na mboga mboga hayapaswi kutunzwa pamoja
Baadhi ya matunda hutoa kemikali iitwayo ethylene yanapoanza kuiva. Matunda yanayotoa kemikali hii ni kama vile ndizi mbivu, matikiti, mapea, embe, nyanya, na tende.
Shida inakuja kwamba baadhi ya matunda na mboga mboga kama vile matufaha, mbilingani, matikiti, viazi mviringo, maboga, karoti, na sukumawiki huathiriwa na kemikali hii.
Matunda haya huanza kuoza kwa haraka yanapoguswa na kemikali hii. Kwa hivyo jenga tabia ya kuyatenganisha na mboga hizi katika makundi tofauti.
 
Baadhi ya matunda na mboga mboga hayapaswi kutunzwa pamoja
Baadhi ya matunda hutoa kemikali iitwayo ethylene yanapoanza kuiva. Matunda yanayotoa kemikali hii ni kama vile ndizi mbivu, matikiti, mapea, embe, nyanya, na tende.
Shida inakuja kwamba baadhi ya matunda na mboga mboga kama vile matufaha, mbilingani, matikiti, viazi mviringo, maboga, karoti, na sukumawiki huathiriwa na kemikali hii.
Matunda haya huanza kuoza kwa haraka yanapoguswa na kemikali hii. Kwa hivyo jenga tabia ya kuyatenganisha na mboga hizi katika makundi tofauti.
 
Acha mazoea ya kuchanganya nyanya na vitunguu
Ukienda sokoni viungo maarufu ni nyanya na vitunguu.
Na mama na dada zetu huvibeba kwa pamoja na kuvitunza pamoja. Hii haishauriwi. Kama ukitunza vitunguu na nyanya mahali pamoja, vitunguu huanza kuota.
Tunza nyanya sehemu yake na vitunguu sehemu yake.
 
Tunza vitunguu maji na vitunguu saumu mahali penye giza
Vitunguu saumu na vitunguu maji havipendi mwanga. Vinapenda giza!
Fanya hivi ili kufifanya vidumu kwa muda mrefu:
Pangusa vitunguu hivi kwa kitambaa au tishu
Chukua mfuko wa karatasi au chombo cha plastiki kisha toboa matundu madogo madogo kwenye vifaa hivi
Viringisha vitunguu ndani ya vitambaa kisha tumbukiza ndani ya mfuko au chombo kilichotobolewa
Tunza mahali popote (kwenye kabati au jokofu sehemu ya baridi kidogo).
Utakuwa umetimiza mahitaji ya vitunguu maji na vitunguu saumu kutaka kuachwa gizani
 
Tunza viazi mviringo mahali pasipo na mwanga
Miale ya jua ni adui wa viazi mviringo. Usitunze viazi mviringo mahali ambako miale ya jua inafika. Hii husababisha kuanza kuoza.
Badala yake tunza katika sehemu kavu na giza katika vyombo kama vile platiki au maboksi ya mbao.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…