Watu watatu wamefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu wakikabiliwa na mashtaka matano likiwamo la kukutwa na ndege watatu aina ya Tausi wa Ikulu ya Jijini Dar es Salaam wenye thamani ya Tsh.Milioni 3.4.
_
Watu hao ambao ni David Graha, Mohamed Hatibu na Mohamed Ally wamefikishwa Mahakamani hapo na kusomewa mashtaka yao mbele ya Hakimu Mkazi Vick Mwaikambo.
_
Baada ya kusoma maelezo hayo, upande wa Serikali umeeleza kuwa upelelezi wa shauri hilo bado haujakamilika, hivyo wanaomba tarehe nyingine kwa ajili ya kutajwa.
_
Hakimu Mwaikambo amesema kwa kuwa mashtaka yanayowakabili washtakiwa hayana dhamana watakwenda rumande, kesi itatajwa tena Novemba 7, mwaka huu.
#MillardAyoMAHAKAMANI