Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

IMG-20191025-WA0013.jpeg
 
NJAA MWANA MALEGEZA SHIBE MWANA MALEVYA.

Na Thadei Ole Mushi.

Kauli ya Kigwangala ni ya kweli kabisa, kweli isiyonashaka ila najiuliza kauli kama hizi vijana ambao wamemaliza vyuo wanaichukuliaje? Je maisha kwao kuwa magumu ni Upumbavu wao? Je wananchi wa Kule Nzega anakotokea Kigwangala wanajisikiaje?

Huyu ni waziri, mtumishi wa umma ambaye anasubiria mshahara kama watu wengine, analipiwa Makazi, Usafiri,na posho kibao na fedha hizi zinatoka kwa hao hao wenye maisha Magumu, kauli kama hii ingetolewa na Bakharesa, au Mo tungesema anawainspire vijana kupambana kwa kuwa hawa wanajitegemea wenyewe hawategemi ajira wamejiajiri si kama Kigwangala.

Kuna watu walilima Korosho wakaishia kuzila, kuna watu walilina Pamba wanaishia kuziangalia kwenye magodown nk. Hawa kwao maisha ni magumu je nao tuwajumuishe kwenye upumbavu wao? Kigwangala anaongea sana..... tukimwondoa kwenye huo utumishi wa Umma ndio ataelewa kauli za wananchi kuwa maisha ni magumu kweli kweli.

Huyu ni waziri kashalewa kiyoyozi cha V8 atakuwa kaamkia kwenye Hotel ya Kifahari huko Mbugani na hangover zake sasa anaona wenye maisha Magumu ni wapumbavu. Shibe nayo ina ulevi wake.

Ole Mushi.
0712702602
 
Back
Top Bottom