Pamoja na kuonyesha soka ya kuvutia, Emery alimtoa kipindi cha pili na kuibua maswali kwa wachambuzi akiwemo nguli wa zamani wa Liverpool, Jamier Carragher.
Muangalie Ozil alivyocheza kwa kiwango kile, si kipenzi cha mashabiki lakini anastahili kuanza katika kikosi cha kwanza Arsenal,”alisema beki huyo wa zamani wa England.
Nyota huyo wa Ujerumani alitoa mchango wa mabao matatu kabla ya kutoka katika mchezo huo uliozalisha idadi ya mabao 10, baada ya kutoka sare ya 5-5. Liverpool ilisonga mbele kwa ushindi wa penalti 5-4.
Aliyekuwa mkufunzi wa Manchester United na Chelsea Jose Mourinho yuko tayari kurudi katika soka ya Uingereza kutokana na lengo lake la kutaka kushinda mataji katika ligi ya Premia. (Sky Sports)
Manchester City inataka kumsajili Jadon Sancho kutoka klabu ya Borrusia Dortmund , lakini mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 19 ambaye alikuwa katika chuo cha mafunzo ya kandanda katika klabu ya City kabla ya kuelekea Ujerumani atagharimu zaidi ya £100m. (Sport Bild, via Sport Witness)
Mkurugenzi mkuu wa klabu ya LA Galaxy Dennis te Kloese ana mipango ya kukutana na Zlatan Ibrahimovic, 38, kujadili hatma ya mshambuliaji huyo kwa lengo la kumzuia kutoondoka katika klabu hiyo. (ESPN)
Juventus iko tayari kumuuza mshambuliaji wa Croatia Mario Mandzukic, 33, kwa Manchester United au Sevilla mwezi Januari , lakini wanataka kulipwa dau la £4.6m. (Calciomercato, via Mirror)
Wolves na Watford wanajiandaa kuwasilisha ombi la kumnunua beki wa kulia wa klabu ya Royal Antwerp na Ureno Aurelio Buta 22 ifikiapo mwezi Januari kwa dau la £5m. (Mail)
Ajenti wa Bale , Jonathan Barnett, amefutilia mbali uvumi kwamba raia huyo wa Wales anatarajiwa kuondoka Real Madrid na kujiunga na klabu moja ya China . (Independent)
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.