Mchezaji wa kimataifa wa Ufaransa na Paris St-Germain, Kylian Mbappe, 20, siku moja ataichezea Real Madrid, kwa mujibu wa rais wa klabu ya Monaco Vadim Vasilyev. (Mail)
Kiungo wa kati wa Barcelona Mhispania Carles Alena,21, anayelengwa na Tottenham huenda akaruhusiwa kuondoka klabu hiyo kwa mkopo mwezi Januari mwakani. (Mundo Deportivo - in Spanish)
Bayern Munich inapania kumsaini winga wa Manchester City Leroy Sane, lakini iko tayari kulipa euro milioni 80 pekee (Β£69m) kumpata kiungo huyo wa kimataifa wa Ujerumani. (Calciomercato)
Barcelona na Manchester City wako tayari kumenyana katika kinya'nganyiro cha usajili wa kiungo wa kati wa Uruguay na Juventus, Rodrigo Bentancur, 22. (Star)
habari za sungura zinamuhusu depal kwa sababu mahari yake ni sungura 30.
cha ajabu davet amezigeuza hadithi za sungura kuwa tamthilia ya isidingo.
tokea asubuhi sunguraaa mpaka muda huu sunguraaaa