Inadhaniwa kwamba malimau yalikuzwa kwanza Kusini-mashariki ya Asia. Lakini baada ya muda, yalisafirishwa hadi upande wa magharibi, kuelekea bahari ya Mediterania. Milimau hukua vizuri katika eneo lenye baridi na joto la kiasi, na kwa sababu hiyo, miti hiyo hukua vizuri sana huko Argentina, Hispania, Italia, Mexico, na hata sehemu za Afrika na Asia.