AKINA MAMA NA AKINA DADA CHUKUENI TAHADHALI:
IGP Simon Siro amekiri kwamba sambamba na wimbi kubwa la utekaji wa watoto, jeshi la Polisi sasa hivi linapambana na wimbi jingine kubwa la kubakwa kwa akina mama na akina dada kinakofanywa na watu wanaojifanya ni madereva bodaboda. Amesema watu hao hujifanya wanaendesha boda boda na wanapokodiwa na akinamama au akina dada huwapeleka kwa lazima maeneo ya maficho na kuwabaka.
Matukio haya yajaripotiwa sana na vyombo vya habari kwa sababu wanaobakwa mara nyingi huogopa kuuhabarisha umma kwamba wamebakwa, lakini huwa wanaripoti polisi kimya kimya, na wimbi la wanaoripoti polisi kwa kubakwa linazidi kuongezeka kila siku.
Ningewashauri akina mama na akina dada kuhakikisha kama wanakodi boda boda wahakikishe ni dereva wanayemfahamu. Bora uchelewe unakokwenda kwa kumsubiri dereva bodaboda unayemfahamu hata kama umempigia simu akakwambia yuko mbali, kuliko kupanda bodaboda ya mtu usiyemfahamu halafu ukabakwa.
Tuwafahamishe mama zetu, dada zetu na binti zetu kokote tunakoweza kuwafikia.