Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Usiku wa juzi Jumatano kwenye Ligi ya Mabingwa Ulaya, Manchester City ilihitaji huduma ya beki wake, Kyle Walker kuwajibika kama kipa baada ya mwenye nafasi hiyo, Claudio Bravo kutolewa kwa kadi nyekundu kwa kumchezea rafu Josip Ilicic wa Atalanta akiwa mtu wa mwisho.
 
Kipa namba moja wa Man City, Ederson alitolewa wakati wa mapumziko na kuingia Claudio Bravo, ambaye alionyeshwa kadi nyekundu zikiwa zimebaki dakika 10. Kocha Pep Guardiola alitazama kwenye benchi lake na kumwinua beki wa kulia, Walker kwenda kuziba pengo la Bravo uwanjani,
 
Harry Kane – Tottenham vs Asteras Tripoli, 2014

Harry Kane hakuwa huyu Kane anayefahamika kwa sasa kipindi hicho, Oktoba 2014. Alikuwa bado ni mchezaji wa kawaida sana kwenye kikosi cha kwanza cha Tottenham. Kwenye mechi moja ya Europa League, dhidi ya Asteras Tripoli, kipa Hugo Lloris alitolewa kwa kadi nyekundu dakika tatu kabla ya filimbi ya mwisho na hapo Spurs ilikuwa imemaliza sub zake, ikalazimika Kane kuwa kipa. Kane alishindwa kudaka shuti la Jeronimo Barrales, mpira ukiponyoka mikononi na kuwa bao. Kabla ya kuwa kipa, Kane alikuwa amefunga hat-trick kwenye mechi hiyo kuisaidia Spurs kushinda 5-1. Erik Lamela alifunga mawili.
 
9) John Terry – Chelsea vs Reading, 2006

Kumpoteza kipa mmoja kwa majeruhi kwenye mechi ni bahati mbaya, lakini kumpoeza kipa wa pili ndani ya mechi hiyo hiyo ni mkosi. Hilo lilitokea wakati Chelsea ilipokipiga na Reading, 2006 na Petr Cech alijigonga na Stephen Hunt akaumia akatolewa uwanjani, kisha akaingia Carlo Cudicini, ambaye pia aliumia baada ya kugongana na Ibrahima Sonko. Baada ya hapo, beki wa kati John Terry akalazimika kwenda kuwa kipa na kumalizia dakika zilizokuwa zimebaki kwenye mchezo huo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…