Kelechi Iheanacho
Leicester City ilifanikiwa kuinasa huduma ya Kelechi Iheanacho mwaka 2017 na kuzipiku klabu za Tottenham, West Ham na Monaco. Staa huyo alitokea Manchester City, ambako aliondoka na kuacha timu yake huko nyuma ikionyesha Liverpool ubabe na kubeba ubingwa wa Ligi Kuu England mwaka uliofuatia.
Lakini, wakati inamuuza, Man City iliweka kipengele kwenye mkataba wake kwamba kwa vyovyote Iheanacho atakavyokuwa kwenye ubora, basi timu hiyo itakapohitaji saini yake basi itumie Pauni 50 milioni tu kumrudisha mchezaji huyo Etihad bila ya kujali thamani yake atakayokuwa nayo sokoni kwa wakati huo