Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Je wajua mimea ina akili kuliko unavyofikiri?

1. Mimea ina uwezo wa kuwasiliana na wadudu.

Utafiti unaonyesha mimea ina uwezo wa kuwasiliana na wadudu. Mpaka sasa tafiti zinaonyesha zinathibitisha mimea kuwasiliana na wadudu. Viwavi wanapoushambulia mmea, mmea hutengeneza na kutoa aina fulani ya kemikali inayowavuta wadudu wanaokula viwavi, kuja ulipo mmea na kuanza kumla yule mdudu hivyo mmea huo kujilinda.

Imagine hata wewe unapopumzika kwenye mti, mara unashangaa sisimizi kibao wanakufuata kukusumbua. Maybe mimea huwaita....

2. Mimea ina kumbukumbu

Tafiti zinaonyesha mimea ina uwezo wa kuhusianisha wavelength za mwanga. Watafiti wanadai ukiumulika mti kwa mda wa saa na ukau expose na virusi, hutengeneza kemikali fulani inayopambana na virusi hao. Hivyo, wakati mwingine utakapoumulika tena kwa mda wa saa na mwanga uleule, hutengeneza na kuitoa kemikali hiyo kwa ajili ya kupambana na virusi. Utafiti huu unakazia, hayo yanaonyesha jinsi mimea ilivyo na kumbukumbu.

Narudi!!!
 
Lakini, wachezaji hao hakuna atakayepatikana kwa pesa ndogo, wote wanahitaji mkwanja mrefu kuwanasa kitu ambacho kitamfanya kocha huyo azidi kuliweka jina lake juu zaidi katika orodha ya makocha waliotumia pesa nyingi kusajili mastaa wapya kwenye maisha yao ya ukocha.
 
Unai Emery – Pauni 634.23 milioni

Kocha wa Arsenal, Unai Emery amepata sifa ya aina yake akiwa ndiye mtu aliyemsajili Neymar kwa pesa iliyovunja rekodi ya dunia wakati alipokuwa huko Paris Saint-Germain. Mchezaji huyo amemgharimu Pauni 199 milioni alipomnasa kutoka Barcelona. Lakini, Emery ni moja ya makocha waliotumia pesa nyingi katika kunasa wachezaji wapya, ambapo kwenye kipindi chake cha ukocha amenasa wachezaji 63 katika timu sita tofauti alizozinoa na kumgharimu Pauni 634.23 milioni. Akiwa Arsenal, timu imetumia pesa nyingi kumsajili Nicolas Pepe, lakini imewanasa pia David Luiz na Kieran Tierney kwa mkwanja mrefu. Kocha huyo aliwahi kupita pia Sevilla na Valencia alikotumia pesa kusajili.
 
Rafael Benitez – Pauni 677.42 milioni

Rafael Benitez amejitengenezea jina lake vyema kwa kipindi chake alichotamba alipokuwa na kikosi cha Liverpool ambapo alibeba taji la Ligi ya Mabingwa Ulaya. Lakini, kocha huyo Mhispaniola ametumia pesa nyingi pia kwenye usajili wa wachezaji wake, ambapo kwa ujumla amenasa mastaa 92 katika timu saba tofauti alizowahi kufanya kazi na wamemgharimu Pauni 677.42 milioni. Lakini, wachezaji 10 kati ya 14 aliowanasa kwa pesa nyingi alifanya hivyo akiwa Anfield, ambapo Fernando Torres alikuwa mmoja wao alipomnasa kwa Pauni 34 milioni. Mchezaji mwingine ghali aliyemnasa ni Gonzalo Higuain, Pauni 35 milioni kutoka Real Madrid wakati huo akiwa Napoli.
 
Claudio Ranieri – Pauni 720.93 milioni

Claudio Ranieri aliwaduwaza wengi wakati alipoigeuza Leicester City kuwa timu iliyokuwa ikipewa nafasi kubwa ya kushuka daraja hadi kwenda kubeba ubingwa wa Ligi Kuu England. Lakini, kocha huyo Mtaliano, naye anafahamika vyema kwa kutumia pesa nyingi kwenye dili za usajili. Kwa ujumla wake, Ranieri amesajili wachezaji 95 katika timu 11 tofauti alizowahi kuzinoa na kutumia Pauni 720.93 milioni. Wachezaji wake wa pesa nyingi zaidi aliwahi kuwasajili ni wakati wake aliokuwa Monaco, alipowanasa James Rodriguez na Radamel Falcao kwa karibu Pauni 80 milioni. Alitumia pesa nyingi pia kwa kipindi chake alichokuwa Chelsea na Juventus.
 
Roberto Mancini – Pauni 721.41 milioni

Wachezaji saba kati ya 10 ambao Roberto Mancini aliwasajili kwa pesa nyingi alifanya hivyo akiwa na kikosi cha Manchester City ambacho alikiunda vyema na kuwaongoza kubeba taji lao la kwanza la Ligi Kuu England. Wachezaji ghali zaidi wa Mancini ni Sergio Aguero (Pauni 36 milioni) na Edin Dzeko (Pauni 33 milioni). Kwa ujumla wake katika maisha yake ya ukocha, Mancini amesajili wachezaji 79 akiwa na timu sita tofauti na wachezaji hao wamemgharimu Pauni 721.41 milioni. Mwaka 2015 alipokuwa na kikosi cha Inter Milan alimsajili kiungo Geoffrey Kondogbia kwa ada ya Pauni 32.4 milioni na kuwa mchezaji ghali aliyemsajili nje ya Man City. Sasa anainoa Italia.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…