Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Roberto Mancini – Pauni 721.41 milioni

Wachezaji saba kati ya 10 ambao Roberto Mancini aliwasajili kwa pesa nyingi alifanya hivyo akiwa na kikosi cha Manchester City ambacho alikiunda vyema na kuwaongoza kubeba taji lao la kwanza la Ligi Kuu England. Wachezaji ghali zaidi wa Mancini ni Sergio Aguero (Pauni 36 milioni) na Edin Dzeko (Pauni 33 milioni). Kwa ujumla wake katika maisha yake ya ukocha, Mancini amesajili wachezaji 79 akiwa na timu sita tofauti na wachezaji hao wamemgharimu Pauni 721.41 milioni. Mwaka 2015 alipokuwa na kikosi cha Inter Milan alimsajili kiungo Geoffrey Kondogbia kwa ada ya Pauni 32.4 milioni na kuwa mchezaji ghali aliyemsajili nje ya Man City. Sasa anainoa Italia.
 
Massimiliano Allegri – Pauni 914 milioni

Max Allegri ni bonge la kocha kwenye mchezo wa soka. Anafahamu vyema namna ya kushinda mataji na jambo hilo lilimfanya anase pia huduma ya staa anayependa kushinda mataji, Cristiano Ronaldo. Lakini, kwa sasa kocha huyo Mtaliano hana kazi tangu alipoachana na Juventus mwishoni mwa msimu uliopita. Kwenye maisha yake ya soka, Allegri amesajili jumla ya wachezaji 87 akiwa na timu tatu tofauti na kumgharimu Pauni 914 milioni. Ronaldo ndiye mchezaji aliyemsajili kwa pesa nyingi, Pauni 105 milioni. Wachezaji wengine aliowanasa kwa mkwanja mrefu ni Gonzalo Higuain, Joao Cancelo, Paulo Dybala na Federico Bernardeschi. Kwa sasa anasubiri kazi mpya.
 
Manuel Pellegrini – Pauni 949.14 milioni

Kocha wa West Ham United, Manuel Pellegrini amebakiza pesa kidogo sana kugota kwenye Pauni bilioni za matumizi yake kwenye kunasa wachezaji wapya katika maisha yake ya soka. Kama ilivyo kwa Allegri, mchezaji wake ghali zaidi kuwahi kumsajili ni Cristiano Ronaldo, aliyemgharimu Pauni 84 milioni mwaka 2009 alipomng’oa Manchester United kipindi hicho akiwa Real Madrid. Kisha alimnasa kiungo Kevin De Bruyne huko Manchester City kwa pesa nyingi kabisa, huku uhamisho wa Kaka kutoka AC Milan kwenda Real Madrid, nao ulikuwa wa pesa nyingi. Kwa ujumla wake, Pellegrini amesejili zaidi ya wachezaji 82 akiwa na timu nane tofauti kwa Pauni 949.14 milioni.
 
Arsene Wenger – Pauni 867.38 milioni

Huyu ndiye mtu anayewasababishia matatizo mengi makocha wapya wanaokuja kwenye kikosi cha Arsenal. Mfaransa huyo, Arsene Wenger aliifanya Arsenal kupata mafanikio makubwa ndani ya uwanja na kuacha pengo kubwa sana alipoondoka, ambapo kocha wa sasa Unai Emery haonekani kuwa na uwezo wa kuliziba. Katika maisha yake ya ukocha, Wenger amesajili wachezaji 103 na kutumia Pauni 867.38 milioni. Wachezaji wake waliomgharimu pesa nyingi ni Pierre-Emerick Aubameyang, Alexandre Lacazette, Mesut Ozil na Grant Xhaka, ambao wote aliwasajili akiwa na kikosi cha Arsenal. Wachezaji hao wote hakuna hata mmoja aliyemsajili kwa dau chini ya Pauni 40 milioni.
 
Pep Guardiola – Pauni 1.03 bilioni

Mhispaniola, Pep Guardiola ni kocha wa tatu kutumia mabilioni ya pesa kunasa saini za wachezaji wapya. Kocha huyo kwa ujumla wake amesajili wachezaji 52 katika timu tatu alizowahi kufanya kazi na kutumia Pauni 1.03 bilioni. Na kitu cha kisichoshangaza ni kwamba wachezaji saba kati ya nane aliowasajili kwa pesa nyingi amefanya hivyo akiwa na kikosi cha Manchester City, ambako alipata nguvu ya bodi ya wakurugenzi kumletea wachezaji anaowataka. Huko nyuma mchezaji aliyekuwa amemsajili kwa pesa nyingi ni Zlatan Ibrahimovic wakati huo alipomnasa kwa Pauni 62.5 milioni kutoka Inter Milan mwaka 2009. Kisha wachezaji waliomgharimu pesa nyingi ni kiungo Rodri.
 
Carlo Ancelotti – Pauni 1.11 bilioni

Kwenye orodha ya makocha wenye mafanikio makubwa kabisa huko Ulaya, Carlo Ancelotti ni mmoja wao, ambapo ameshinda mataji matatu ya Ligi ya Mabingwa Ulaya na mataji mengine kibao ya ligi. Nyakati zake alizokuwa kwenye kikosi cha Los Blancos, kocha huyo Mtaliano alifungua pochi kunasa mastaa wa maana, akiwamo Gareth Bale, aliyemgharimu Pauni 90 milioni na James Rodriguez kwa Pauni 67.5 milioni.
 
Jose Mourinho – Pauni 1.40 bilioni

Jose Mourinho anafahamu kitu gani cha kufanya kushinda mechi na mataji na kwa kutambua hilo, amekuwa akijitahidi kwa nguvu zote kunasa wachezaji mahiri duniani. Rekodi zake zinaonyesha kwamba yeye ndiye kocha aliyetumia pesa nyingi zaidi kwenye kunasa wachezaji, Pauni 1.4 bilioni tangu alipoanza ukocha.
 
Wapi, Saint anne.
Njoo tuendelee na shangwe zetu
FB_IMG_1574529374080.jpeg
 
Hebufikiri ukinunua kiwanja sehemu ambayo ni mkondo wa maji au udongo wake unatitia; hili litakulazimu kutumia gharama kubwa zaidi ili kukifanya kiwanja hicho kifae kwa ujenzi, gharama ambazo zingeweza kuokolewa kama ungefanya uchaguzi sahihi wa kiwanja.
 
Back
Top Bottom