Massimiliano Allegri – Pauni 914 milioni
Max Allegri ni bonge la kocha kwenye mchezo wa soka. Anafahamu vyema namna ya kushinda mataji na jambo hilo lilimfanya anase pia huduma ya staa anayependa kushinda mataji, Cristiano Ronaldo. Lakini, kwa sasa kocha huyo Mtaliano hana kazi tangu alipoachana na Juventus mwishoni mwa msimu uliopita. Kwenye maisha yake ya soka, Allegri amesajili jumla ya wachezaji 87 akiwa na timu tatu tofauti na kumgharimu Pauni 914 milioni. Ronaldo ndiye mchezaji aliyemsajili kwa pesa nyingi, Pauni 105 milioni. Wachezaji wengine aliowanasa kwa mkwanja mrefu ni Gonzalo Higuain, Joao Cancelo, Paulo Dybala na Federico Bernardeschi. Kwa sasa anasubiri kazi mpya.