Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Tunafahamu jinsi inavoleta usumbufu kwa tumbo kujaa gesi maana kila mara utahitaji kwenda chooni kujisaidia na kujamba, licha ya usumbufu huu ,tatizo la tumbo kujaa gesi inaweza kuwa ni kiashiria cha matatizo makubwa ya kiafya mfano fangasi kwenye mfumo wa chakula.
 
Dalili za Tumbo Kujaa Gesi

Kuwa na gesi tumboni ni tofauti kabisa na kitambi, kitambi kinaweza kuwa cha muda mrefu lakini tumbo la gesi ni la muda tu baadae husinyaa na kurudi katika hali ya kawaida kwani huletekezwa na hewa kukwama tumboni na kufanya tumbo kutanuka. Kwa watu wengine tumbo linaweza kuwa kubwa kama mjamzito.
 
Kwa bahati nzuri ni kwamba tatizo la gesi tumboni unaweza kulitatua ukiwa nyumbani kwako kwa kurekebisha tu mpangilio wa lishe yako. kwa kesi chache mfano kama tatizo linakutokea mara kwa mara basi kuna haja ya kupanga appointment ukaonana na dactari kwa vipimo. Dalili zingine zinazoambatana na tumbo kujaa gesi ni kama
 
Homa
Muwasho kwenye koo, machozi
Kukosa choo au kupata choo kigumu na kuharisha
Uwepo wa damu kwenye hajakubwa au mkojo
Kupungua kwa uzito kusiko kawaida
Maumivu kwenye sehemu za tezi hasa kwenye koo na kwapa
Mwili kukosa nguvu na uchovu sana
Kuvurugika kwa hedhi
Bawasiri
Ubongo kutofanya kazi vizuri
 
Maji kubakizwa mwilini (fluid retention)
Wkati fulani maji yanaweza kuabakizwa kwenye sehemu fulani za mwili kama kweye magoti, tumboni na kwenye nyonga. Maji haya huletekeza maumivu makali kwenye joints na tumboni. Uwepo wa maji tumboni hujulikna kama Ascites na inaweza kuashiria kwamba una tatizo kwenye ini au maambukizi ya bacteria. Ndio maana kuna umuhimu wa kuanya vipimo kama una homa ya ini (hepatitis B). kama kuna shida ya ini basi utapata dalili zingine kama kichfuchefu, macho na ngozi kuwa njano, kupungua uzito, kutapikadamu na chakula kutosagwa tumboni.
 
Mwili kukosa maji (Dehydration)
Umewahi kufuatilia siku ukiwa umekunywa sana pombe ama kula zaidi vyakula vyenye chumvi kwa wingi na tumbo likajaa gesi?. Mwili unapokosa maji hufanya uchakataji na usagaji wa chakula kuwa mgumu. mwili unapokosa maji ya kutosha basi hufanya kazi ya kuvuta na kuhifadhi maji mengi zaidi pale utakapokunywa maji ili kuepuka kutokea kwa upungufu huu, maji yanapokuwa mengi kupita kiasi ndipo sasa unaweza kupata choo kigumu ama kukosa choo. hakikisha unakunywa maji mara nyingi zaidi kila siku ili kuepuka tumbo kujaa gesi.
 
Constipaton
Constipatina inaweza kuwa sababu kubwa ya kwanini tumbo lijae gesi. constipation inaweza kusababisha choo kigumu, maumivu tumboni na kukosa choo kwa muda mrefu. Constipationa husabishwa na ulaji wa vyakula vilivyokobolewa sana visivyo na kambakamba, matumizi kidogo ya maji, msongo wa mawazo na kuishi bila kufanya mazoezi.
 
Alegi ya Chakula
Alegi ya vyakula mbalimbali kama maziwa, mayai na ngano vinaweza kuwa ni sababu ya kujaa gesi kwa tumbo lako. Kuna aina nyingi ya vyakula inaweza kusababisha upate mzip ama alegi, cha kufanya sikiliza mwili wako unasemaje pale unapokula chakula, kama mwili unkataa aina fulani ya vyakula na unapata mcharuko kama kuvimba,kuhrisha, ama kutapika basi usitumie chakula hicho.
 
Majeraha Kwenye Mfumo wa Chakula
Wakati mwingine unaweza kupata gesi tumboni kutokana na vidonda ama uvimbe kwenye baadhi ya sehemu za mfumo wa chakula kama utumbo mdogo na utumbo mpana. Uvimbe unaweza kuzuia utolewaji wa uchafu na kuletekeza gesi na maji kukwama.
 
Mabadiliko ya Homoni
PMS (pre menstrual syndrome) ikimaanisha mkusanyiko wa dalili zisizo za kawaida za kipindi cha hedhi ni chanzo cha tumbo kujaa gesi. Tatizo linaweza kuwa kubwa kama una uvimbe kwenye kizazi na hedhi yako inavurugika. Kwanini wanawake hupata gesi tumbo wakati au karibia na kipindi cha hedhi? Mwanamke anapokaribia hedhi kiwango cha homoni ya estrogen huongezeka na ukuta wa mfuko wa mimba kuongezeka. Pale anapopata siku zake basi damu na maji mengi hutolewa nje na hivo tumbo kurudi katika hali ya kawaida.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…