Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
Bro habari za Uzima vipi maendeleo wewe na familia
[emoji1][emoji1][emoji1]salama kabisa ndugu yangu. Habari ya siku nyingi?
Tunaendelea vizuri kabisa. Wewe je?
Samahani ule mfumo anautumia binti yetu, nitakuona kwa mfumo mwingine.
 
STAA, Raheem Sterling yupo kwenye mazungumzo ya kunasa dili jipya huko Manchester City ambalo litamfanya awe mchezaji anayelipwa pesa nyingi kuliko yeyote huko Etihad. Anaripotiwa kwamba dili hilo mpya litamfanya Sterling alipwe Pauni 450,000 kwa wiki.
 
10. Jurgen Klopp (Pauni 134,615 kwa wiki)

Baada ya kuwapa ubingwa wa Ligi ya Mabingwa Ulaya, Liverpool huwaambii kitu kuhusu kocha wao Mjerumani, Jurgen Klopp. Huduma yake bora anayotoa huko Anfield ilimfanya awindwe na klabu kadhaa za huko Ulaya, lakini Liverpool wanapambana kwa kila hali kuhakikisha anabaki, ikiwezekana kumpa mshahara mkubwa zaidi, ambapo kwa sasa analipwa Pauni 7 milioni kwa mwaka. Lakini, mkwanja huo unaingia kwenye akaunti ya Klopp kila wiki, Pauni 134,615.
 
Barcelona ni moja ya timu ambazo zimeingia kwenye orodha ya klabu 10 Ulaya zinazowalipa mishahara mikubwa makocha wao. Wababe hao wa Nou Camp wananolewa na Ernesto Valverde, ambaye kwa kila mwaka wanamwingizia kwenye akaunti yake ya benki, Pauni 8 milioni. Kocha huyo aliyepata bahati ya kumnoa staa wa dunia, Lionel Messi jambo hilo linaendana na mshahara wake ambapo kwa kila wiki anavuna Pauni 153,846. Si pesa ya mchezomchezo.
 
8. Thomas Tuchel (Pauni 153,846 kwa wiki)

Kwa kocha yeyote anapoambiwa kwamba anatafutwa na Paris Saint Germain bila ya shaka atakuwa mwenye furaha kubwa kwa sababu anafahamu wazi anakwenda kuchukua kazi ya pesa ndefu. Si unajua timu hiyo inamilikiwa na matajiri wa Kiarabu, hivyo suala la kulipwa mshahara mkubwa sio tatizo na kocha Tuchel kwa mwaka anaweka mfukoni Pauni 8 milioni. Tuchel yupo vizuri, kwenye akaunti yake ya benki inaingizwa mshahara wa Pauni 153,846 kwa wiki.
 
7. Antonio Conte (Pauni 173,077 kwa wiki)

Conte alipofutwa kazi huko Chelsea, alikaa kijiweni kwa muda kidogo kabla ya kwenda kuikamatia kazi ya kuinoa Inter Milan. Ajira hiyo iliyomrudisha kwao Italia, imemfanya Conte kutokuwa na maisha ya kinyonge kwa sababu mshahara wake anaolipwa ni mzuri, Pauni 9 milioni zinaingia kwenye akaunti yake ya benki kwa mwaka. Lakini, kitu kitamu zaidi kwake ni kwamba mkwanja huo analipwa ka kila wiki, ambapo ndani ya siku hizo saba, Conte anaweka mfukoni Pauni 173,077.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…