Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Kwa hakika Kitabu hichi ni kidogo basi. Lakini, kama alivyosema muandishi kuwa kaandika kwa ufupi, bali ufupi wa kutosheleza faida yake. Yoyote atakaye kisoma kitabu hichi kwa kutaka kufahamu na bila ya mawazo yake kudhibitiwa na kupenda au kuchukiya, basi hapana shaka atapata faida
 
Atafahamu jinsi wananchi wa Zanzibar walivyokuwa katika harakati zao za kuwania uhuru wa nchi yao kutokana na ukoloni wa Muingereza. Harakati ambazo zalianza kabla ya miaka ya 1940. Pia ataweza kufahamu ni nani walioanzisha harakati hizo, namna zilivyopata kuungwa mkono na wananchi na namna zilivyokuwa zikiendeleya. Pia atapata kufahamu jinsi ya pingamizi zilivyokuwa
 
Pia atafahamu vipi wananchi chini ya uwongozi wa vyama vyao ZNP/ZPPP walivyokuwa wakizikabili pingamizi hizo. Na zaidi atafahamu juhudi za waongozi wa ZNP/ZPPP katika kutaka mafahamiano na ushirikiano na wananchi wenziao ASP na nini ulikuwa muelekeo wa waongozi wa ASP, muelekeo ambao mara nyingi ulikuwa ukiathirika kwa uwongozi na fikra zilizokuwa zikipangwa na kuletwa kutoka nje ya nchi.
 
Chungutamu. Kweli ni chungu! Lakini ni wajibu isemwe na kubainishwa. Uchungu uliyomo ndani ya kitabu hichi ni kuona jinsi wananchi walivyohangaika kwa jasho, mali na hata damu zao kwa kuwania uhuru wao kutokana na ukoloni wa Muingereza, lakini kwa sababu ya husda, chuki na ufisadi uhuru huo haukuachiwa kuishi zaidi ya siku thalathini! Isitoshe, sio kuwa uhuru huo ulipotezwa kwa kutumiliwa njiya za usalama, sivyo, bali kwa fujo! Fujo ambalo natija yake ni kupotezwa Dola ya Zanzibar,
 
roho za wananchi, heshima ya binaadamu, mali za watu na mwisho kuwachwa wananchi kuishi ndani ya haramu. Utamu japo kwa hakika sio utamu ni kwa vile kuweza wananchi kupata kuufahamu UKWELI ambao kwa muda wa zaidi ya miaka thalathini umekuwa ukifunikwa kwa UWONGO. Lakini, kama yalivyo maumbile, kweli daima huibuka.
 
Nimelichagua jina hili la UKWELI NI HUU KUUSUTA UWONGO, baada ya kuyasikia na kuyasoma me ngi ya uwongo na hata yakafika kusomeshwa watoto wetu katika maskuli ya Zanzibar kukhusu hayo yenye kuitwa "MAPINDUZI" yaliyofanyika katika visiwa vyetu vya Zanzibar mnamo taarikh 12 Januari 1964.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…