D A E M U S H I N
JF-Expert Member
- Dec 15, 2015
- 22,665
- 121,102
Kuanzia chumba cha tisa mpaka cha 12, na baada ya muda katika miaka ya 1950 kuanzia chumba cha saba mpaka cha 12, wazee walitakiwa wasaidie kitu kidogo katika masomo ya watoto wao. Malipo hayo yalikuwa ya kitu kidogo sana na si kila mzee alikuwa akilipa ada hizo. Wengi sana katika wazee walikuwa hawalipi hata senti moja. Na hao waliokuwa wakilipa, wengi wao walikuwa wakilipa kuanzia Shs. tano mpaka Shs. 20 kwa wingi kila baada ya miezi mitatu au mine.