Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

niache nisome kitabu angalau na mimi nijisifu mbele ya hadhira.......
haya waliosoma vitabu mwaka 2019 wajitokezeee
  1. pandu ngozi: nimesoma vitabu 50
  2. shazume: nimesoma vitabu 45
  3. bibi kipini: nimesoma vitabu 40
  4. daemusin mnywaji urojo : nimesoma nusu kitabu
Hivyo vitabu si vya darasa la kwanza mpendwa huko zanzibar
 
HIZBU KUMLETA ZANZIBAR SEYYID ABDULRAHMAN (BABU)
Miezi michache kabla ya uchaguzi wa mwanzo wa 1957, Chama cha HizbulWattan kilimleta Babu Zanzibar ili ashirikiane na wananchi wenziwe katika harakati za kisiasa. Baada ya kufika Zanzibar, Hizbu ilimteuwa kuwa Katibu Mtendaji wa Chama (Excutive Secretary). Kutokana na maarifa aliyokuwa nayo katika mipango ya kuendesha chama cha kisiasa, Babu baada ya muda mdogo alianzisha Umoja wa Vijana (Youth Own Union) (YOU).
1575194309544.png
 
Kwa msaada na ushirikiano wa waongozi wenziwe na wananchi Babu alifanya kazi kubwa katika kukijenga Chama cha Hizbu ndani na nje ya nchi. Lakini, kwa bahati mbaya, kama alivyokuwa hodari katika kukijenga, ndivyo alivyojaribu kwa uhodari au ilivyo khasa kwa kiujanja kutaka kukibomoa baada ya kushindwa kufikilia maslahi yake binafsi kwa kukitumilia chama. (Baadae tutaeleza aliyoyatenda katika kukibomoa chama na kuifisidi nchi).
 
Alipojiunga Sheikh Ali Muhsin katika chama cha HizbulWattan Zanzibar Nationalist Party (ZNP) aliwapa shauri wakuu wa Chama kumtaka Babu achukue mafunzo katika kuendesha chama na baadae aje asaidie katika uendeshaji wa ZNP. Wakuu wakapendezewa na shauri hiyo, na Babu akawafik. Sheikh Ali hapo tena aliiomba Labour Party ya huko Uingereza kwa kupitia kwa (wasta wa) Mr. John Hatch na Mrs. Eirene White M.P. na Labour Party ikakubali kumpokea Babu kwa mafunzo.
 
Mafunzo hayo yalikuwa ya muda wa miezi sita. ZNP (Hizbu) ililipia gharama zote za kimaisha kwa muda huo na za safari. Katika muda huo pia aliendelea kulipwa mshahara akiwa ni Executive Secretary wa Chama ZNP. Utaona dhahiri kuwa imani ya Hizbu juu ya elimu na maarifa haikufungika sehemu mmoja tu, bali ilikuwa ni kwa kila upande. Hizbu iliamini kuwa uwongozi mwema wa chama na nchi utapatikana kutokana na watu wenye ujuzi na maarifa, kwa hivyo iliona umuhimu wa kumpatia mafunzo na elimu ifaayo Katibu Mtendaji wake khasa, na wengine wafuatie
 
NATIJA YA SAFARI YA SHEIKH ALI MUHSIN Kama tulivyoeleza hapo mwanzoni kuwa Sheikh Ali Muhsin alizitembelea baadhi ya nchi za Ulaya pamoja na Uingereza kwa ajili ya kugombania kupatikana kwa mabadiliko ya Katiba ya Kuanzishwa kwa uchaguzi wa "Common Roll" yaani "One Man One Vote" katika Zanzibar. Natija ya safari hiyo, Serikali ya Kiingereza, ilimleta Zanzibar Mr. Coutts akiwa ni mchunguzi juu ya maendeleo ya Katiba. Mchunguzi huyo alifika Zanzibar kati ya mwaka wa 1956. Chama cha Hizbu kilifanya maandamano makubwa kwa kumpokea Mr. Coutts hapo kiwanja cha Ndege cha Kiembe Samaki siku aliyofika Zanzibar. Waandamanaji walichukuwa mabango yaliyokuwa yameandikwa:
"TUNATAKA UCHAGUZI WA ONE MAN ONE VOTE" "TUNATAKA UHURU WA NCHI YETU" "TUMECHOKA KUTAWALIWA'' ''TUNAPINGA "UBAGUZI WA RANGI NA WA UKABILA"
 
Mjumbe huyo alipokuwa nchini alikutana na wananchi pamoja na wakaazi mbali mbali wa nchini. Alionana hata na watu binafsi. Na alipokea risala (za maandishi na za mdomo) kutoka vyama mbali mbali vya kikabila na vya kidini. Chama cha Hizbu nao walionana na mjumbe huyo na walimkabidhi risala yao yenye kutilia nguvu matakwa yao, matakwa ambayo ndio msingi wa ujumbe wake wa kuja Zanzibar. Inafaa ifahamike kuwa tangu kufika kwa mchunguzi huyo na mpaka kuondoka hapakuwepo chama cha kisiasa nchini isipokuwa kimoja tu HizbulWattan. Vyama vyote vya kisiasa vyengine viliasisiwa baadae. Kwahivyo HizbulWattan ndicho chama cha mwanzo cha kisiasa kuasisiwa Zanzibar.
 
Mr. Coutts alipomaliza shughuli zake alirejea kwao. Baada ya muda alileta mapendekezo ya uchunguzi wake kwa Balozi wa Serikali ya Kiingereza aliyekuwepo Zanzibar. Katika mapendekezo yake hayo, Mr. Coutts alikubali kuwa Zanzibar inafaa kuanzishwa uchaguzi wa "Common Roll" yaani uchaguzi wa kwa pamoja, bila ya kujali khitilafu za kabila.

Lakini alipendekeza kuwa uchaguzi uanzie kwa viti sita na vilivyobakia viendelee katika mpango ule ule wa kuteuliwa na Balozi wa Serikali ya Kiingereza kwa kushauriana na Mfalme wa nchi. Pia katika mapendekezo yake, Bwana Coutts alitaka Balozi wa 14 Kiingereza aendelee kuwa Mwenye Kiti wa Baraza la Kutunga Sheria na watumishi wa Serikali ya Kiingereza waendelee kuwa waongozi wa upande wa Serikali.
 
Hizbu haikuridhika hata kidogo na mapendekezo hayo, kwa vile asli ya madaai yao ni kuwa Wawakilishi wote wa Baraza la Kutunga Sheria wawe ni wananchi waliyo chaguliwa na wananchi kwa uchaguzi wa "One Man One Vote". Juu ya hivyo, Hizbu ilikubali kushiriki katika uchaguzi huo kwa kuona kuwa msingi wa matakwa yao ulipatikana; nao ni kuanzishwa kwa uchaguzi wa "Common Roll".

Kwa kukubaliwa misingi hii Zanzibar ikawa ndiyo nchi ya mwanzo katika Afrika Mashariki, Afrika ya Kati na ya Kusini kuanzishwa uchguzi kama huo. Baada ya kupatikana haya HizbulWattan ilizidisha juhudi za kuwafahamisha wananchi misingi na faida ya kuchaguwa Wawakilishi wao kwa kupitia uchaguzi huo.
 
WAKOLONI NA NYERERE NDIO WAASISI WA AFROSHIRAZI
Wakuu wa Serikali wa Idara ya Utawala, Zanzibar baada ya kuona kuwa mpaka kuondoka kwa mchunguzi Coutts Zanzibar na mpaka kuleta mapendekezo ya uchunguzi wake, hapakuweza kuasisiwa chama chengine cha kisiasa nchni ili kipate kushindana na HizbulWattan (ZNP), waliamua kumtumilia Mwalimu Julius Kambarage Nyerere.

Wakoloni walimtumilia Mwalimu kwa kuja Zanzibar kujaribu kuwashawishi waongozi wa vyama viwili vya kikabila waweze kuungana na kuasisi chama kimoja cha kisiasa ili kiweze kushiriki katika uchaguzi na kiweze kuwa pingamizi kwa Chama cha Hizbu. Katika ripoti ya Mr. Penny aliyekuwa Muangalizi wa Uchaguzi aliandika, "Ofisi yangu na Idara ya Utawala zilisaidia kuundwa kwa AfroShirazi na kwahivyo ikaokolewa Zanzibar na kuwa na utawala wa chama kimoja wa namna ya khatari."
 
Mwalimu Nyerere alikuja Zanzibar pamoja na Sheikh Zubeir Mtemvu mnamo mwisho wa mwaka 1956. Mwalimu pamoja na ujumbe wake alikutana na waongozi wa African Association, Sheikh Abeid Amani Karume, Bwana Mtumwa Borafia na Bwana Boniface. Waongozi wa Shirazi Association aliokutana nao Nyerere katika ujumbe wake huo ni, Sheikh Ameir Tajo, Sheikh Thabit Kombo Jecha na Sheikh Othman Shariff Musa. Mkutano huo ulifanyika katika nyumba ya Sheikh Abeid Amani Karume iliyokuwepo mtaa wa Kachorora, Mwembe Kisonge.
 
Nyumba hiyo kwa wakati huo, ilikuwa ikikaliwa na Maalim Haji Ali Mnoga na Bwana Hija Saleh Hija. Njama hizo za wakoloni pamoja na Mwalimu Nyerere zilifanikiwa. Taarikhi 2 Februari 1957, miezi michache tu kabla ya kufikia uchaguzi wa mwanzo wa Juni, 1957 Chama cha AfroShirazi kiliasisiwa rasmi (kikiwa ni muungano wa jumuiya mbili za kikabila yaani "African Association na Shirazi Association").
 
Karume akawa Rais wa chama, Sheikh Ameir Tajo Makamo wa Rais na Sheikh Thabit Kombo Katibu Mkuu. Uwongozi wa chama haukwenda kwa mzalendo, haukwenda laa kwa Sheikh Ameir Tajo walaa kwa Sheikh Thabit Kombo, walaa kwa Sheikh Othaman Shariff, bali kwa Mzee Karume. Mbinu na njama za kuuwangamiza Uzanzibari zilianzwa zamani.
 
UCHAGUZI WA MWANZO JUNI 1957
Kutokana na mapendekezo ya uchunguzi wa Bwana Coutts kukhusu uchaguzi, uchaguzi wa mwanzo ulifanyika, June, 1957. Na kwa uchaguzi huo ndio wananchi wa Unguja na Pemba kwa mara ya kwanza waliweza kushiriki katika kuwachagua Wawakilishi wao wa Baraza la Kutunga Sheria la nchi yao. Uchaguzi huu ulikuwa wa viti sita. Majimbo mane yalikuwa kwa Unguja na mawili Pemba.

Majimbo sita hayo yaligaiwa kama hivi:
Unguja: Majumba ya Mawe
Unguja: N'gambo
Unguja: Kaskazini Unguja:
Kusini Pemba:
Kaskazini Pemba: Kusini
 
Sheikh Ali Muhsin alisimama katika jimbo la N'gambo akiwa ni Mwakilishi wa HizbulWattan, akishindania na Sheikh Abeid Karume akiwa Mwakilishi wa AfroShirazi, na Sheikh Ibuni Saleh alisimama katika jimbo hilo hilo akiwa ni mgombea huru. (independent candidate). Bwana Rutti Bulsara alisimama katika jimbo la Majumba ya Mawe akiwa Mwakilishi wa Hizbu na washindani wake wakiwa, Bwana Choudhry, Mwakilishi wa Muslim Association, Bwana Anverali Hassan Virji, mgombea huru na Bwana AbdulQadir 15 Mukri, akiwa naye pia ni mgombea huru.
 
KWENYE SHARI HUZALIWA KHERI Kushindwa HizbulWattan katika uchaguzi wa mwanzo, ndiko kuliko zidi kuwazinduwa wananchi na kujitokeza paruwanja katika kusimama bega kwa bega na wananchi, wazalendo wenziwao katika juhudi za kuigomboa nchi yao kutokana na ukoloni wa Kiingereza. Baada ya kumalizika kwa machofu ya pirika pirika za uchaguzi, Chama cha Hizbu kilitayarisha mkutano maalumu wa hadhara katika Jumba la Seyyid Khalifa Hall (sasa ati linaitwa "Karume House").

1575195355861.png
 
Kwa jinsi mabibi walivyokuja kwa wingi kwenye mkutana huo, ililazimu wanaume wote waliyokuwemo katika ukumbi wa jumba hilo watoke nje kwa kuwapisha mabibi. Wanaume, wao walikaa katika uwanja wa Bustani ya jumba hilo. Siku hiyo ndipo wanawake walipodai wawe na Sehemu yao katika Chama, na wapate kura sawa na wanaume.

Waliopiga kifua mbele kati yao ni BiZuhura bt Saleh, 16 BiSharifa Ahmed na BiZamzam Sultan. Kuanzia siku hiyo, kila usiku uchao, wananchi wake kwa waume walikuwa wakijitokeza kwa wingi katika kujiunga na Chama cha Wazalendo wenziwao. Waongozi wa chama kwa kulingana na umma unavyozidi kujiunga na chama kila siku ilibidi watengeneze mipango kukhusu kueneza mafunzo na siasa ya chama kila upande
 
KUGAWANYIKA KWA AFROSHIRAZI
Mwanzoni mwa 1959 kulitokea mgawanyiko wa waongozi wa Chama cha AfroShirazi. Sheikh Mohammed Shamte na Sheikh Ali Shariff waliamua kujitoa katika chama na kwa kutoka kwao, kulifuatiwa na wanachama wengi nyuma yao khasa Pemba. Katika wakati huo huo, Chama cha AfroShirazi kilimfukuza katika chama Sheikh Ameir Tajo kwa singizio la kuwa alikwenda kuwaombea msaada wa fedha vijana wa YASU (Young African Social Union) kwa Sir Tayabali Karemjee kwa ajili ya ujenzi wa klabu (club) yao iliyokuwepo Miembeni, bila ya kuiarifu kamati kuu ya AfroShirazi.
 
sababu kubwa zilizompelekea Sheikh Mohammed Shamte na wenziwe kujitoa katika Chama cha AfroShirazi ni zenye kutokana na hisia za uwananchi khalisi kwa nchi yake. Hisia zake za kisiasa na nyendo zake pamoja na matarajio yake juu ya nchi yake yalikuwa ya kutaka kutumikia upatikane uhuru wa Zanzibar. Uhuru utaongozwa na Wazanzibari wenyewe bila ya kuchukua amri au shauri kutoka pahala pengine popote.
 
Back
Top Bottom