D A E M U S H I N
JF-Expert Member
- Dec 15, 2015
- 22,665
- 121,102
Kwa kuhudhuriya mazungumzo ya Uhuru huko London, Hizbu ilitengeneza mipango maalum ili baadhi ya waongozi wa Chama nawo wawepo huko London wakati wa mazungumzo hayo ya Uhuru. Miongoni mwa waliokuwepo huko ni Babu akiwa ndiye Katibu Mtendaji wa Chama, Suleiman Malik na mimi Aman Thani tukiwa ndio wenye dhamana ya Ofisi ya ZNP iliyokuwepo Cairo wakati huo.