Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Saleh Saadalla alikuwa taabani kwa kuambiwa maneno kama hayo na mtu ambaye wakati alipokuwa na uheshimiwa wake alikuwa hawezi hata kumkurubia licha ya kuzungumza naye. Katika nyoyo zetu mlichanganyika baina ya kuhisi kuwa anastahiki kuambiwa maneno kama hayo na baina ya kumuonea huruma, kwani machozi yalikuwa yakimlengalenga, kwa uchungu na kujiona jinsi alivyodhulumiwa, tena kudhululmiwa kwenyewe alikofanyiwa na mwenziwe waliotoka mbali pamoja. Kwa hakika wakati huo alikuwa anahitajia rehema kuliko kustahiki masusuiko, kwani alikuwa hana hila wala uwezo.

Baada ya Saleh kutumikia kifungo chake kwa muda, siku moja tulipoamka na kuanza kugaiwa kazi, mwenzetu hatukumuona na ndio ikawa hatukumuona tena hadi hii leo. Kutokana na khabari zenye kuaminika tulizozipata kutoka kwa baadhi ya wachungaji wetu wa magereza zilisema kuwa Saleh Saadalla alichukuliwa na waheshimiwa wenzake mnamo pingapinga za usiku, alipelekwa Chukwani na 60 huko ndiko alikouliwa kwa kupigwa risasi na kutoswa baharini kama alivyotoswa Othman Shariff
 
 
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…