Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Katika maneno aliyoyasema mbele ya wafungwa, alisema na khasa akimkusudia ndugu yake Mdungi Usi Maalim Nngwali Usi. Maalim Nngwali wakati huo tulikuwa naye pamoja gerezani akiwa miongoni mwa wafungwa wa serikali ya mavamizi.

Karume alimwambia Maalim Nngwali, "
Wewe tumekufanyia kila kheri; mpaka tumekupeleka nchi za nje kusoma, lakini hukuweza kuthamini kitu ila kufuata ufisadi wa kaka yako (yaani Mdungi Usi). Haya leo kaka yako tushamuondoa duniani, utamfuata huko aliko!?" Alipokuwa akisema, "

tushamuondoa duniani", Karume aliupitisha mkono wake kwenye shingo yake kuonesha kuwa ameuliwa (amekatwa roho). Ujabari ulioje huu wa Karume, kuuwa na kujisifu!!
 
71c956918f1ce82616d754aa0db9a084.jpg
 
ALIYONIZUNGUMZIYA TWALA
Mimi na Bwana AbdulAziz Twala kabla ya kuwa watumwa wa Karume na Serikali yake ya Mavamizi katika magereza yake hatukupata kuwa na maingiliano ya namna yoyote. Lakini baada ya kuishi pamoja huko utumwani, tulikuwa masahibu wakubwa kama watu tuliokuwa na maingiliano tangu zamani. Maslahi ya nchi yetu ndio yaliotukusanya pamoja. Tulikuwa kila siku baada ya kumaliza kutumwa na kumaliza kutafuna mapande yetu ya muhogo mchungu na majani mapevu ya muhogo (ati kisamvu),

tulikuwa tukitafuta upenu na kukaa kwa mazungumzo. Mazungumzo yetu makubwa yalikuwa juu ya kufikiri mustakbali wa nchi yetu Zanzibar kwa kutokana na namna ya Karume alivyokuwa akiendesha nchi. Twala alikuwa na imani kubwa juu yangu hata alifika kunihadharisha na baadhi ya wenzake kama Jaha Ubwa, Mdungi Usi na Said Tumba (Said Njugu). Na wao kwa upande wao walimhadharisha yeye Twala kukhusu mimi. Walimwambia, "Tunakuona unaambatana na Aman, lakini usisahau kuwa ni Mhizbu". Twala alikasirishwa na maneno hayo, na aliwafahamisha juu ya fikra zao potofu hizo. Naye alinieleza yote walioyokuwa wakimwambia.
 
YALOMFIKA OTHMAN SHARIFF
Twala ameniambia kuwa tokea kuasisiwa Umoja wa Vijana wa YASU na Othman Shariff kuwa ndiye Rais wa Umoja huo, Karume alikuwa hamtizami Othman kwa jicho la rehema. Kwa vile Karume alivyojiona hakubahatika kuwa katika wasomi, na kuwa Othman alikuwa ni msomi, akifikiria kuwa siku moja Othman ataweza kuchukua uwongozi juu ya Waafrika. Na hilo, Karume alikuwa sitayari kulikubali. Twala alisema kuwa kwa kuyakinga hayo, khatua za mwanzo alizochukuwa Karume baada ya kufaulu kwa Mavamizi ya Zanzibar ni kupiga marufuku vyama vyote tokea vya kisiasa mpaka vya kijamii (Social) na vya kikabila, na YASU ikiwa moja wapo. Khatua ya pili alimuondoa Othman na kumpeleka katika nchi za nje kuwa Balozi wa Tanzania.
 
Karume alitawala kwa mkono wa chuma sana. Nimekuta stori kati, vipi kuhusu Abdallah Kassim Hanga? Ushamjadili
kule kwetu joseon ya zamani alikuwepo mwanadamu mmoja anaitwa lee bang won.
aliua ndugu zake
aliua macomrades wake
aliua mashemegi
aliua wakwe zake na marafiki zake

huku zanzibar nafasi hiyo ilibebwa na karume
 
Twala ameniambia, katika mwaka 1966, Othman Shariff alikuja Tanzania kwa kazi za Serikali na baada ya kumaliza kazi zake DaresSalaam, alitembelea Zanzibar. Hakutimiza muda mkubwa ila ghafla tulimuona Othman ameletwa katika kikao cha mkutano wa Baraza la 'Mapinduzi'. Twala anasema kuwa Karume aliwaambia, "Nimemleta huyu fisadi mbele yenu, juu ya kumfanya Balozi wa Serikali yetu huko Marekani, bado hajatoshelezeka anataka lazima awe yeye ndiye Rais wa nchi hii. Vitimbi vyake vyote anavyovifanya vya kutaka kutuletea fujo na michafuko katika nchi yetu ili apate kuwarejesha mabwana zake,

tumevipata kwa ukamilifu kabla yeye mwenyewe kufika Tanzania. Alipofika hapa vijana wa kazi walikuwa wakimuandama katika kila njia zake bila ya yeye mwenyewe kufahamu. Katika nyendo zake, vijana wa kazi wamemuona ana jishughulisha na kuvitembelea baadhi ya vituo vyetu vya kijeshi, na alikuwa akijaribu kuwatomasa tomasa baadhi ya wanajeshi wetu ili waweze kuwa upande wake hapo atapokuwa tayari kuufanya huo ufisadi wake. Vijana wa kazi walipomuona amefika kiasi hicho, walimtia mbaroni na kumleta kwangu, na mimi sasa namleta mbele yenu kwa kutaka uwamuzi wenu nini tumfanye"
 
Twala ameniambia kuwa wengi kati yetu tulipigwa na msangao kwani tulikuwa na hakika kuwa aliyokuwa akiyasema Karume yalikuwa maneno ya uwongo, lakini nani ataweza kuuliza au kumkaidi au kumhoji. Mwisho mwenyewe alitoa uwamuzi wake wa kumfunga gerezani Othman Shariff kifungo cha miaka kumi! Twala ameniambia kuwa, hapo hapo Karume aliwapa amri Ibrahim Makungu na Edington Kisasi wamchukue Othman Shariff kumpeleka gerezani kwa kuwa ndiyo keshahukumiwa. Twala alipokuwa akinizungumzia hayo, nilidawaa. Nilimuuliza Twala, "Kwani katika hilo Baraza lenu mlikuwa hamna haki ya kusema au kuuliza? Basi palikuwa na faida gani ya kuitana na kukutana?" Kwangu miye kuyasikiya haya hayakuwa ya ajabu kwani serikali hii kuwazuliya watu uwongo wananchi ndio misingi ya siasa yake. Huwazulia uwongo wakawafunga, wakapokonya vyoa bali hata wakawachukulia ahli zao. Huko magerezani wakawatia vilema kwa mateso na wengine wakawauwa.
 
Back
Top Bottom