D A E M U S H I N
JF-Expert Member
- Dec 15, 2015
- 22,665
- 121,102
Baada ya kumaliza kuwafukia hao wenziwao, waliambiwa, "Nyie siku yenu kesho. Tutakumalizeni kama tulivyowamaliza hawa wenzenu. Leo mtarudi gerezani na kesho mtaletwa tena hapa. Tunakwambieni, hatutaki kusikia mmesema lolote katika haya yaliyopita hapa hii leo. Walirejeshwa gerezani katika hali mbaya sana kwani walikuwa kama wamerukwa na akili kwa khofu zilizowajaa kwa kushuhudia ukatili kama huo wakitendewa wenziwao. Mungu ndiye Mungu, wao walijiona ndio wenye uwezo wa kufanya kila walitakalo. Walisahau kuwa Mwenye Enzi Mungu ndiye mwenye nguvu na ndiye muweza wa kufanya atakalo. Wananchi hao waliyobakia, hawakupelekwa kwenda kumalizwa kama walivyoambiwa