Waziri wa Maliasili na Utalii Dkt. Hamisi Kigwangalla @hamisi_kigwangalla amesema ni kazi sana ku-respond kwenye matakwa ya Watanzania ““Ama kweli Wabongo huwa hatujui tunachotaka, ni kazi sana ku-respond kwenye matakwa yetu sisi watanzania, wengine walianza kurusha mawe kwa Serikali kuwa hatutumii fursa za uwepo wa wasanii, tulipowatumia, wakalalamika, na wengine wakasema tunakula Bata tu!”
_
“Wengine wakalalamika kuwa Rwanda inatupita sababu wanatumia soka kujitangaza, tukarespond, kufanya utafiti na uchambuzi wa kina wa njia hii ya kujitangaza kama inalipa ama la, na kama tuingie ama laah!, Majuzi Rwanda kaongeza mkataba mwingine tena, mkatushambulia”- KIGWANGALLA
_
“Mkatushambulia kuwa tumelala, tuna vivutio vingi, iweje Rwanda atupite kujitangaza? Rwanda wako strategic zaidi yetu! Nikaona niwaeleze kuwa nasi hatujakaa kimya, kuna proposal nyingi tumeletewa, kama Serikali tuna utaratibu rigorous wa kufanya uamuzi, tunachambua”-KIGWANGALLA
_
“Nikasema tunashughulikia taarifa tulizonazo, tukiona kuna faida kwetu kuwekeza pesa ya serikali, tutaingia huko, kama hakuna hatutoingia, nayo imekuwa tena mbaya, tusiige Rwanda, Kwa nini tusubiri mpaka clubs zitufuate? N.K, la wema lipi ndugu zangu?”- WAZIRI KIGWANGALLA