Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Beki Maguire, ambaye alikuwa nahodha wa Man United kwenye ushindi huo wa Jumamosi, alisema: “Top Four sasa tumeanza kuiona, lakini yatupaswa kuendelea kupambana kupata matokeo haya. Kuanzia mwezi uliopita au zaidi, nikiwa beki nimekuwa nikiwaangalia washambuliaji na kuamini watatupigia tu mabao ya ushindi.
 
Wale watu wetu wanne kwenye kipindi cha kwanza walikuwa na njaa. Walikuwa tishio kubwa kwa wapinzani, hakika walionyesha ukomavu kwa wapinzani. Naamini sasa wameanzna kuelewana. Lakini, tusibweteke na kujihasau, ule ulikuwa mshindi mkubwa na pointi tatu muhimu, tunapaswa kuendelea kufunga mabao.”
 
Maguire, 26, aliongeza: “Tunaona kabisa mwaka huu kwenye baadhi ya mechi hatukupata matokeo ambayo yalistahili kunyakua pointi tatu. Lakini, kwa mechi mbili zilizopita, sidhani kama kuna mwenye kutia shaka kuhusu matokeo ya ushindi tuliyopata, tulistahili.”
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…