Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Washirika wabaya wa kibiashara

Mshirika mzuri wa kibiashara ni yule anayeweza kukuunga mkono katika maono na malengo yako ya kibiashara. Biashara nyingi hufanya kazi na washirika wabaya wasioweza kuendeleza maono na malengo ya biashara husika; hili husababisha biashara nyingi kukwama kwa kukosa ushirikiano stahiki.
 
Mambo yasiyo ya kiuchumi

Kuna mambo yanayoweza kuua biashara ambayo mengi siyo ya kiuchumi na mara nyingi hayazuiliki. Maswala kama vile majanga ya asili (mafuriko, ukame, tetemeko n.k), mabadiliko ya hali ya uchumi wa nchi na dunia, sera mbovu za kisiasa, vita, n.k. Ni baadhi ya mambo ambayo yanaweza kusababisha biashara kufa. Pamoja na hali hii biashara mbalimbali zinaweza kuweka mipango mapema ya kujiokoa katika hali hizi kama vile kuhakikisha uwepo wa akiba ya kutosha ya rasilimali hasa fedha
 
Mbinu duni za masoko

Masoko ni taaluma rasmi inayofanywa na watu waliofuzu vyema. Ni tatizo kubwa sana kupuuza swala la masoko. Biashara nyingi hazifahamu jinsi ya kutafuta na kutawala soko, hivyo hujikuta wakipoteza soko la bidhaa zao na hatimaye kufa kwa kukosa mapato. Ni muhimu kujifunza mbinu sahihi za masoko kulingana na bidhaa na wakati husika
 
Kuajiri watumishi duni

Biashara nyingi hupendelea watumishi duni (cheap labour) ili wawalipe malipo kidogo. Ni ukweli usiopingika kuwa mtumishi duni atafanya kazi duni. Biashara nyingi hazioni mafanikio wala matokeo chanya, kutokana na kuajiri watu wasiokuwa na uwezo wala ubunifu wa kufanya biashara husika kwa njia yenye tija. Ni heri kuajiri mtumishi mmoja bora kuliko watano duni.
 
Matatizo ya kisheria

Kuna wakati biashara au kampuni huingia kwenye matatizo ya kisheria yanayoigharimu biashara au kampuni husika fedha nyingi. Migogoro na matatizo haya yanaweza hata kupelekea kufilisiwa kwa biashara husika. Kwa mfano kampuni ya Shell ilikumbana na kesi mbalilimbali ikiwemo ya uchafuzi wa mazingira iliyoigarimu zaidi ya dola za kimarekani 291,000. Kesi hizi zimeiathiri Shell kwa kiasi kikubwa hadi kufunga vituo vyake sehemu mbalimbali duniani. Ni muhimu kuzingatia sheria katika ufanyaji wa biashara ili kuepuka kutumbukia kwenye matatizo kama haya.
 
Mipango duni

Ili ufanikiwe katika biashara unahitaji mpango mzuri wa biashara. Biashara nyingi zinazoanzishwa Afrika hazina mipango madhubuti ya kibiashara inayoonyesha maswala kama vile muundo wa utawala, mtaji, mikakati au mipango ya mauzo, n.k Biashara nyingi pia hukosa lengo; jambo ambalo hufanya biashara nyingi kufa.
 
Uongozi na usimamizi mbaya

Kufanikiwa kwa biashara kunategemea usimamizi mzuri. Uwekaji wa mipango na kuisimamia ili itimie hufanywa na uongozi mzuri. Ni wazi pia rasilimali nyingi za kampuni zitapotea kutokana na kukosa uongozi na usimamizi mzuri. Biashara nyingi za Afrika huendeshwa kwa mazoea au kuendeshwa na watu wenye uwezo mdogo katika utawala.
 
Kupuuza wateja na mahitaji yao

Naamini unafahamu msemo usemao kuwa “Mteja ni mfalme”. Biashara nyingi za kiafrika hufa kutokana na kupuuza wateja pamoja na mahitaji yao. Unaweza kuona mfanyabiashara anamjibu mteja vibaya au hamkaribishi kwa furaha bila sababu yoyote ya msingi. Wakati mwingine wafanyabiashara hawasikilizi maoni na mahitaji ya wateja jinsi ipasavyo. Mfanyabiashara kujihisi kuwa yeye ndiyo mwenye faida kwa mteja ni kosa kubwa litakalogarimu biashara yake.
 
Kutokujifunza kutokana na makosa

Makosa ni shule muhimu inayotuwezesha kuboresha viwango vya utendaji. Ni wazi kuwa yapo makosa yanayofanyika mara kwa mara kwenye uendeshaji wa biashara. Wakati mwingine makosa haya huleta athari mbaya kwa biashara. Wafanyabiashara wengi hawapendi kujifunza kutokana na makosa haya ili wayaepuke mbeleni; hivyo yanapotokea tena huwakuta hawajajiandaa vyema.
 
Kujipanua bila mipango

Upanuzi wa biashara ni jambo linalohitaji mipango madhubuti. Kuongeza ukubwa wa biashara kunahitaji kutazama mambo kama vile mtaji, watumishi, vitendeakazi, uendeshaji na usimamizi, masoko n.k. Biashara nyingi hujipanua bila kutazama mambo haya; jambo ambalo linapelekea biashara nyingi kufa.
 
Eneo baya la kibiashara

Uchaguzi mbaya wa eneo la kibiashara hupelekea biashara nyingi kufa kutokana na kukosa wateja. Biashara nyingi hushindwa kubainisha eneo ambalo linafaa kwa ajili ya biashara zao na hatimaye hukosa wateja na kufa. Kwa mfano kufungua biashara ya kuuza vifaa vya magari katikati ya soko la vyakula ni wazi kuwa mauzo yatakuwa duni sana.
 
Back
Top Bottom