Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

6. Claudio Ranieri – mechi 187

Claudio Ranieri amefanya kazi kwenye timu tatu tofauti ndani ya Ligi Kuu England, huku moja ya mafanikio makubwa aliyapata akiwa na Leicester City alipobeba ubingwa wa Ligi Kuu England. Kocha huyo aliwahi kufanya kazi pia Chelsea na baadaye Fulham.
 
Kwenye Ligi Kuu England, kocha Rafa Benitez amepata bahati ya kuzinoa timu kadhaa akianzia Liverpool kisha Chelsea na baadaye Newcastle United. Huko Anfield maisha yake yalikuwa matamu ikiwamo kushinda ubingwa wa Ligi ya Mabingwa Ulaya na taji la Kombe la FA.
 
Kwenye kikosi cha Chelsea pia mambo yake hayakuwa mabaya kihivyo. Lakini, Mhispaniola huyo ni moja ya makocha waliofanya vizuri kabisa kwenye Ligi Kuu Englanda baada ya kuhitaji mechi 181 tu kufikisha ushindi wa mechi 100 kwenye ligi hiyo.
 
Arsene Wenger – mechi 179

Kuna nyakati nyingi sana nzuri za kocha Arsene Wenger katika kipindi chake cha miaka 22 aliyodumu kwenye kikosi cha Arsenal. Tangu alipoondoka kwenye kikosi hicho viatu vyake vinaonekana kuwa vikubwa, hakuna vinavyomtosha baada ya Unai Emery kuletwa na mambo kumwendelea kombo na sasa ameshafutwa kazi.
 
Wenger ameifanya Arsenal kuwa moja ya timu kubwa kwenye Ligi Kuu England, ikiwahi kucheza kwa msimu mzima bila ya kupoteza mechi yoyote kwenye Ligi Kuu England. Kocha huyo Mfaransa anashika namba nne kwenye orodha ya makocha waliohitaji mechi chache sana za ligi kufikisha ushindi wa mechi 100, akihitaji mechi 179. Kwa sasa Wenger amekuwa mfanyakazi wa Fifa.
 
Sir Alex Ferguson – mechi 162

Si kitu cha kushangaza kumwona Sir Alex Ferguson kwenye orodha hii. Hakuna ubishi, Mskochi huyo ndiye kocha mwenye mafanikio zaidi kwenye Ligi Kuu England kwa kipindi chake alichokuwa huko Manchester United.
 
Kabla ya kujiunga na timu hiyo, Man United ilikuwa timu ya kawaida, lakini Sir Alex aliibadili na kuwa tishio kubwa England ikibeba taji la Ligi Kuu England mara kibao kuanzia 1992/93 hadi hapo alipostaafu mwaka 2013.
 
Sir Alex anashika namba tatu kwa makocha waliotumia mechi chache sana kufikisha ushindi wa mechi 100 kwenye Ligi Kuu England baada ya kutumia mechi 162 kupata ushindi huo. Man United ya Sir Alex ilikuwa moto wa kuotea mbali wakati huo.
 
Jurgen Klopp – mechi 159

Kocha, Jurgen Klopp amekuwa kwenye kiwango bora kabisa huko Liverpool akifanya mambo ya maana na wababe hao wa Anfield. Msimu uliopita, Klopp alishindwa kidogo sana kuwapa Liverpool taji la Ligi Kuu England baada ya kuzidiwa pointi moja tu na Manchester City, lakini msimu huu kila kitu kinaonekana kwenda vizuri upande wao.
 
Upo sawa bro,Kanye katulizwa na Kim,na Kanye anamzimia sana yule dada hyo haina kificho since day one jamaa ameona ile sex tape ya Kim,jamaa anasema aliipa lazima amuweke ndani Kim
Ila ninge kati ya majamaa wooteee kanye kaiwezea familia ya kardashian,hadi now nashangaa hawajamletea mizengwe kama wale wenzie
 
Liverpool ya Klopp imekuwa kwenye kiwango bora na hivyo inamfanya kuwa kocha namba mbili aliyefikisha ushindi wa mechi 100 kwenye ligi hiyo akitumia mechi chache. Klopp alihitaji mechi 159 tu kufikisha idadi hiyo ya mechi 100 za ushindi, hiyo ikiwa ni mara kwenye mechi 59 tu, ndizo ambazo Klopp hakuibuka na ushindi.
 
Jose Mourinho – mechi 142

Jose Mourinho kwa sasa ni kocha wa Tottenham Hotspur ikiwa ni timu yake ya tatu kuinoa kwenye Ligi Kuu England baada ya Chelsea, aliyoinoa kwa awamu mbili tofauti na Manchester United. Kocha huyo amekuwa wa thamani kubwa ndani na nje ya England, akiwahi kuzinoa pia FC Porto ya Ureno, Inter Milan ya Italia na Real Madrid ya Hispania.
 
Alibeba taji la Ligi ya Mabingwa Ulaya mara mbili akiwa na FC Porto na Inter Milan. Akiwa Man United alibeba taji la Europa League. Mourinho ndiye kocha aliyefikisha ushindi wa mechi 100 kwenye Ligi Kuu England akitumia mechi chache zaidi, 142.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…