Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Bro..kwa hiyo yale maua yangu ya alizeti hayana mchongo tena kwa haya sio?
images (1).jpeg
😍😍😍
 
Jumatatu iliyopita, Arsenal ilikuwa na kibarua cha ugenini kwa West Ham United, ambapo ilikuwa mechi ya lazima ushindi baada ya timu kucheza mechi kibao bila ya kushinda. Mchezo huyo, Arsenal ikiwa chini ya Freddie Ljungberg ilifanikiwa kupata ushindi wa mabao 3-1, huku wakitanguliwa kufungwa kwa bao la Angelo Ogbonna kabla ya kinda Gabriel Martinelli kusawazisha na Nicolas Pepe kupiga na pili, kisha Pierre-Emerick Aubameyang akapiga la tatu kuhakikishia timu ushindi.
 
Martinelli kufunga kwenye mchezo huo wa Ligi Kuu England, kitendo hicho kimemfanya kuwa kina wa nane kufunga bao akiwa chini ya umri wa miaka 19 kuwahi kuichezea Arsenal na kudhihirisha bayana sera ya timu hiyo katika kuvuna mambo mazuri kupitia kwa wachezaji makinda.
 
Hii hapa orodha ya makinda wote wa Arsenal waliowahi kuifungia Arsenal kwenye mchakamchaka wa mechi za Ligi Kuu England na kufanya kikosi hicho chenye maskani yake Emirates kutamba kwenye ligi tangu enzi hizo ikiwa na Arsene Wenger hadi sasa ikinolewa na moja ya wachezaji wa zamani wa timu hiyo, Ljungberg baada ya Mhispaniola, Unai Emery kufutwa kazi.
 
Theo Walcott – miaka 18, miezi 11 na siku 7

Arsenal ilipata sare ya 2-2 dhidi ya Birmingham City, Februari 2008 kwenye mchezo wa Ligi Kuu England. Mechi hiyo inabaki kuwa na kumbukumbu ya kudumu kwa sababu ilimshuhudia straika wa Arsenal, Eduardo akivunjika mguu, lakini Theo Walcott naye akifunga bao lake la kwanza kwenye ligi. Theo alifanya hivyo akiwa na umri wa miaka 18, miezi 11 na siku saba. Hiyo ilikuwa mechi yake ya 30 kwenye kikosi hicho na kuliweka jina lake kwenye orodha ya wafungaji. Walcott aliondoka kwenye timu hiyo na sasa anaitumikia Everton.
 
Jack Wilshere – miaka 18, miezi 10 na siku 26

Miaka yake ya mwanzoni kabisa kwenye kikosi cha Arsenal, kiungo Jack Wilshere alionekana wazi kwamba anakwenda kuwa staa mmoja mkubwa sana kwenye timu hiyo. Bao lake la kwanza la Ligi Kuu alifunga kwenye ushindi wa 4-2 dhidi ya Aston Villa, Novemba 2010 na hilo lilipandisha zaidi sifa zake. Wilshere alifunga bao hilo akiwa na umri wa miaka 18, miezi 10 na siku 26 na hivyo kuwa moja wa wachezaji wenye umri mdogo kuifungia Arsenal kwenye Ligi Kuu England. Kiungo huyo Mwingereza aliondoka Arsenal na sasa anaitumikia West Ham United.
 
Nicolas Anelka – miaka 18, miezi saba na siku 26

Arsenal walibeba ubingwa wa Ligi Kuu England msimu wa 1997/98 wakati walipomaliza pointi moja juu ya Manchester United. Hiyo ina maana ushindi wa Arsenal wa mabao 3-2 dhidi ya Man United waliopata Novemba mwaka huo, ulikuwa muhimu kwenye kampeni yao ya kubeba ubingwa. katika mchezo huo, straika Mfaransa, Nicolas Anelka alihitaji dakika tisa tu kufunga bao lake la kwanza kwenye ligi akiwa na umri wa miaka 18, miezi saba na siku 26. Anelka alicheza kwenye timu nyingi sana ikiwamo Real Madrid na sasa amestaafu soka.
 
Aaron Ramsey – miaka 18, miezi 7 na siku 27

Wiki za mwanzo kabisa za msimu wa 2009/10, Arsenal walikuwa kwenye kiwango bora kabisa huku wakiwa na huduma ya kiungo matata, Aaron Ramsey, ambaye alikuwa miongoni mwa waliotikisa nyavu kwenye mchezo wa ushindi wa mabao 4-1 dhidi ya Portsmouth uliopigwa Agosti. Wakati huo, Ramsey alikuwa na umri wa miaka 18, miezi saba na siku 27, alipofunga kwa shuti kali la mbali na hapo mashabiki wakaanza kumtabiria mambo mazuri kiungo sasa. Sasa yupo Juventus, lakini tatizo la majeruhi linamfanya awe nje ya uwanja mara kwa mara huko Italia.
 
Gabriel Martinelli – miaka 18, miezi 5 na siku 21

Gabriel Martinelli ni moja ya makinda matata kabisa walioweka rekodi tamu ya kuifungia Arsenal kwenye Ligi Kuu England. Martinelli alifunga bao la kuwazisha katika ushindi wa 3-1 dhidi ya West Ham United Jumatatu iliyopita. Kinda huyo wa Kibrazili amekuwa moto kwa sasa kwenye kikosi hicho, huku bao lake hilo kwenye ligi alifunga akiwa na umri wa miaka 18, miezi mitano na siku 21. Martinelli pia ni kinda wa kwanza kuanzishwa na Arsenal kwenye ligi na kisha kufunga bao. Ni moja wa makinda wenye uwezo mkubwa waliopo kwenye kikosi hicho kwa sasa.
 
Back
Top Bottom