Aaron Ramsey – miaka 18, miezi 7 na siku 27
Wiki za mwanzo kabisa za msimu wa 2009/10, Arsenal walikuwa kwenye kiwango bora kabisa huku wakiwa na huduma ya kiungo matata, Aaron Ramsey, ambaye alikuwa miongoni mwa waliotikisa nyavu kwenye mchezo wa ushindi wa mabao 4-1 dhidi ya Portsmouth uliopigwa Agosti. Wakati huo, Ramsey alikuwa na umri wa miaka 18, miezi saba na siku 27, alipofunga kwa shuti kali la mbali na hapo mashabiki wakaanza kumtabiria mambo mazuri kiungo sasa. Sasa yupo Juventus, lakini tatizo la majeruhi linamfanya awe nje ya uwanja mara kwa mara huko Italia.