Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Alex Oxlade-Chamberlain – miaka 18, miezi 5 na siku 20

Arsenal iliandikisha ushindi mkubwa sana kwenye historia yao ya Ligi Kuu England wakati walipoichapa Blackburn Rovers 7-1, Februari 2012. Ushindi huo umekuwa na kumbukumbu ya kipekee, kwa sababu kinda wao wa kipindi hicho, Alex Oxlade-Chamberlain alifunga bao lake la kwanza. Wakati anafunga, Alex alikuwa na umri wa miaka 18, miezi mitano na siku 20. Hata hivyo kwenye kikosi cha Arsenal hakuwa akipewa dakika nyingi na sasa anatamba akiwa na Liverpool. Kocha Jurgen Klopp alimchukua Alex na kumfanya kuwa staa mkubwa Anfield.
 
Serge Gnabry – miaka 18, miezi 2 na siku 14

Mwaka 2013, Serge Gnabry alijitambulisha kwenye soka kwamba anakwenda kuwa staa mkubwa wa Arsenal kwa miaka ya baadaye, ambapo ilimchukua mechi tatu tu kufunga bao lake la kwanza kwenye Ligi Kuu England.
 
Wakati anafunga bao hilo, Gnabry alikuwa na umri wa miaka 18, miezi miwili na siku 14, huku akitikisa nyavu kwenye ushindi wa 2-1 dhidi ya Swansea City, Septemba 2013. Hilo lilikuwa bao lake pekee kwenye ligi na sasa anataka akiwa na Bayern Munich. Gnabry alionekana si kitu akaachwa kwenda Bayern, ambako amekuwa tishio.
 
Cesc Fabregas – miaka 17, miezi 3 na siku 21

Wachezaji wengi kwenye orodha hii wametofautiana kwa siku tu, lakini kiungo Mhispaniola, Cesc Fabregas amewazidi wachezaji wenzake kwa zaidi ya mwaka mmoja zaidi akiwa mtoto kuliko wenzake walioweka alama zao kwenye kikosi cha Arsenal, alipofanya hivyo Agosti 2004.
 
Fabregas alifunga bao lake la kwanza la Ligi Kuu England akiwa na umri wa miaka 17, miezi mitatu na siku 21, wakati alipotikisa nyavu kwenye ushindi wa 3-0 dhidi ya Blackburn Rovers. Baada ya kutesa kwa miaka kadhaa akiwa na Arsenal, sasa Mhispaniola huyo yupo Monaco.
 
Hivi culture ni ke au me, mbona analeta vitu vya ajabu sana kwenye hii platform... Nimeona uzi wake akilalamika uzi wwke umefutwa akitia mkazo yale ni maisha yake...kuna watu nati kichwani zime lose
Huyo atakuwa anaishi nje ya nchi ambako mambo hayo ni ya kawaida. Mtaalamu mmoja mbobevu katika mambo ya afya alisema hapa jana kuwa hapa nchini hakuna hospitali inayoweza kufanya hizo ishu za upandikizaji watoto.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…