SHULE 10 GHALI ZAIDI TANZANIA
10. Morogoro International School (MIS)
Ipo Morogoro na hufuata mtaala wa Cambridge. Ada ni kuanzia Tsh milioni 6.4 kwa chekechea hadi Tsh milioni 18 kwa sekondari. Hii ni ada peke yake, mbali na fedha ya usajili na boarding kwa wale wanaolala shuleni.
9. Internation School Moshi (ISM)/ UWC East Africa
Hii ndio shule ghali zaidi katika mkoa wa Kilimanjaro. Ada kuanzia Tsh milioni 16 kwa chekechea hadi Tsh milioni 41 kwa wale wa kidato cha tano na sita. Shule hii hufuata Mtaala wa International Baccalaureate (IB).
8. Aga Khan Primary & Secondary School
Shule hii ipo Dar Es Salaam, na hufuata Mtaala wa IB kama ilivyo ISM. Hutoza ada kuanzia Tsh milioni 7 hadi milioni 20.
7. Haven of Peace Academy (HOPAC)
HOPAC ipo Dar Es Salaam. Hufuata Mtaala wa Cambridge na hutoza ada kati ya Tsh milioni 16 hadi 22 kwa mwaka.
6. Kennedys House Schools
Shule za Kennedys ziko maeneo mengi duniani. Tanzania iko Arusha wakiendesha Chekechea na Shule ya Msingi. Ada zao huanzia Tsh milioni milioni 8 kwa Chekechea hadi milioni 22 kwa Shule ya Msingi. Shule hii hufuata Mtaala wa Cambridge.
5. Saint Constantine International School
Nayo iko Arusha na hufuata Mtaala wa Cambridge. Ada yake ni kati ya Tsh milioni 8 kwa Chekechea hadi Tsh milioni 23 kwa sekondari.
4. Iringa International School (ISS)
Iko Iringa na hufuata mitaala miwili ya IB na ule wa Cambridge. Hutoza ada kati ya Tsh milioni 17 kwa Chekechea hadi milioni 27 kwa sekondari.
3. Dar Es Salaam International Academy (DIA)
Ni shule ya tatu kwa kuwa na ada ghali zaidi nchini. Iko Dar Es Salaam na hufuata Mtaala wa IB. Ada yake kwa mwaka ni kuanzia Tsh milioni 23 kwa shule ya msingi hadi Tsh milioni 40 kwa sekondari.
2. Braeburn International School
Hii iko Dar Es Salaam na Arusha. Hufuata mfumo wa IB na ada yake kwa mwaka ni kuanzia Tsh milioni 20 kwa shule ya msingi hadi Tsh milioni 43 kwa sekondari.
1. International School of Tanganyika (IST)
Hii ndio shule ghali zaidi nchini. Iko jijini Dar Es Salaam na hufuata Mtaala wa IB. IST hutoza ada kuanzia Tsh milioni 34 kwa chekechea hadi shilingi milioni 71 kwa sekondari, kwa mwaka.
USISEME HATUNA HELA SEMA MIMI SINA HELA.