Carragher alisema kwa nafasi anayocheza De Bruyne kwake ndiye mchezaji bora duniani kwa kuwa ana uwezo wa kufanya jambo lolote na wakati wowote uwanjani.
De Bruyne alicheza Genk msimu 2010–2011 kabla ya kujiunga na Chelsea 2012 na baadaye alipelekwa kwa mkopo Werder Bremen kwa kile kilichodaiwa kutokuwa na kiwango bora.
Thamani yake ilipanda na muda mfupi alitua Man City kwa Pauni54 milioni. De Bruyne amecheza mechi zaidi ya mechi 170 akitwaa ubingwa wa Ligi Kuu England mara mbili, mara tatu Kombe la Ligi na moja FA.
De Bruyne amewahi kutangazwa mchezaji bora wa mwaka Man City mwaka 2016 na 2018. Nyota huyo amefunga mabao 28 na 19 katika mechi za kimataifa alizocheza 74.
Licha ya kusifu kiwango bora cha Mason Greenwood, kocha wa Manchester United, Ole Gunnar Solskjaer amesema washambuliaji wake walikosa umakini wa kufunga mabao dhidi ya Everton.
Mason ni mchezaji hodari anajua afanye nini anapokuwa na mpira. Lakini kwa jumla hatukuwa makini katika kumalizia pasi za mwisho, tulipata nafasi tulishindwa kuzitumia kutokana na papara,”alisema Solskajaer.

Ni wachezaji wawili Federico Macheda na Danny Welbeck ndio wachezaji wenye umri mdogo waliowahi kufunga mabao katika mechi za ligi kwenye Uwanja wa Old Trafford wakiwa Man United.
Wachezaji wamecheza kwa kiwango cha juu siwezi kulaumu kwa kupata pointi moja. Nimeridhishwa na namna walivyopambana kuipigania jezi yao. Naamini watafanya hivi msimu mzima,”alisema kocha wa Everton Duncun Ferguson.