Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Maisha ya straika Romelu Lukaku yalikuwa matamu kwelikweli huko Manchester United alipokuwa chini ya kocha Jose Mourinho. Panga pangua Mbelgiji huyo alikuwa kwenye kikosi cha kwanza cha Mourinho akiwa straika chaguo la kwanza la Mreno huyo huko Old Trafford. Lakini, baada ya ujio wa Ole Gunnar Solskjaer tu kwenye kikosi hicho kila kitu kilitibuka, Lukaku akaanza kuchezeshwa pembeni na sio mshambuliaji wa kati tena. Mara akaanza kuonja benchi mechi moja moja kabla ya fowadi huyo kuamua kuondoka kwenye timu hiyo akitimkia zake Inter Milan kabla ya mambo hayajatibuka sana chini ya kocha mpya.
 
Christian Benteke v Jurgen Klopp (Liverpool)

Straika mwingine wa Kibelgiji, Christian Benteke alikuwa moto huko Aston Vila na kuwafanya Liverpool kutoa pesa kunasa saini yake. Maisha yake ya Anfield yalikuwa safi wakati timu hiyo ilipokuwa chini ya Kupatikana kwa huduma ya mshambuliaji huyo kuliwapa Liverpool matumaini ya kufanya vizuri zaidi. Lakini, jambo hilo lilitokea wakati Liverpool ilipokuwa chini ya kocha Brendan Rogers.
 
Hata hivyo, Rodgers alipoonyeshwa mlango wa kutokea na Jurgen Klopp kuja kuchukua mikoba yake, hiyo ilikuwa habari mbaya kwa straika Benteke, ambapo maisha yake hayakuwa mazuri kabisa chini ya kocha mpya. Taratibu akaondolewa kwenye kikosi cha Klopp akachukua wachezaji wake akiwamo Mohamed Salah na Benteke akasukumiziwa Crystal Palace.
 
Rafael da Silva v Louis van Gaal (Man United)

Mashabiki wa Manchester United hawakuelewa kabisa kwanini Louis Van Gaal aliamua kumpiga bei beki pacha wa Kibrazili, Rafael da Silva. Van Gaal alimpiga bei staa huyo kwenda Olympique Lyon na kuwafanya mashabiki wa Man United kushangaa. Lakini, ukweli ni kwamba ni wakati mbaya tu aliokutana nao Rafael chini ya kocha mpya.
 
Kocha Sir Alex Ferguson alikuwa kipenzi kikubwa cha beki huyo mambo yalikuwa hivyo pia chini ya David Moyes, lakini kila kitu kilikuja kuwa tofauti baada ya ujio wa Van Gaal kwenye timu. Rafael alionekana hafai na hivyo kuondoshwa kwenye timu.
 
Joe Hart v Pep Guardiola (Man City)

Timu kibao zilikuwa zikitamani kuwa na huduma ya kipa Joe Hart kwenye vikosi vyao, lakini utashangaa kocha Pep Guardiola alipotua tu Manchester City alimwona kipa huyo hafai. Kwanza akaanza kwa kumtoa kwa mkopo kipa huyo na taratibu akamwondoa kabisa huku akiwaleta kina Claudio Bravo, ambao pia walishindwa kufanya vizuri huko Etihad.
 
Guardiola alifanya usajili wa makipa mfululizo baada ya kumwondoa Joe Hart kwa kumpeleka kwa mkopo Torino na kumnasa Bravo mambo yalikuwa magumu hadi hapo alipofanya usajili wa Ederson, ambaye ndiye chaguo lake la kwanza kwa sasa. Lakini, ukweli wa kuhusu Joe Hart kitendo cha kushindwa kuaminika na Guardiola kilimsababishia matatizo makubwa kisaikolojia na hakuwa fiti tena.
 
Juan Mata v Jose Mourinho (Chelsea)

Mashabiki ulikuwa huwaambii kitu kuhusu kiungo wa Kihispaniola, Juan Mata. Staa huyo alichaguliwa mchezaji bora wa mwaka wa Chelsea kwa misimu miwili mfululizo kabla ya ujio wa kocha Jose Mourinho kurejea kwenye timu hiyo. Mourinho alipotua tu Stamford Bridge katika awamu yake ya pili, mchezaji wa kwanza ambaye aliona kwamba hana nafasi katika timu yake ni Juan Mata, staa ambaye kwa muda wote alikuwa akiwapa burudani kubwa mashabiki wa timu hiyo.
 
Mourinho alianza kumpiga benchi mchezaji huyo na hata alipomchezesha basi haikuwa kwa dakika zote tisini. Baadaye aliamua kumuuza na kuonyesha kwamba hakumhesabia kuwa ni mchezaji hatari, akamuuza kwenda kwa wapinzani wake Manchester United huko Old Trafford, ambako baadaye walikwenda kukutana.
 
Yaya Toure v Pep Guardiola (Man City)

Kiungo Muivory Coast, Yaya Toure alikuwa nembo ya Manchester City kabla ya ujio wa kocha Pep Guardiola kwenye timu hiyo. Panga pangua, Toure alikuwa hakosi kwenye sehemu ya kiungo ya timu hiyo. Lakini, Guardiola alipotua tu, akaanza kumpiga benchi kiungo huyo na kufikia wakati alimwondoa kabisa kwenye kikosi chake cha Ligi ya Mabingwa Ulaya.
 
Jambo hilo liliibua malumbano makubwa kwenye timu na Yaya alisugua sana benchi, shukrani kwa wachezaji wenginne wa sehemu ya kiungo kupata majeruhi na hapo Guardiola hakuna na ujanja zaidi ya kuanza kumtumia mchezaji huyo. Hata hivyo, Yaya hakuwa tena yule aliyekuwa akiwapa raha mashabiki wake na kumfanya aondoke kwenye timu hiyo akiwa na huzuni tofauti na ambavyo angeondoka kabla ya Guardiola kutua kwenye timu hiyo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…