Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Aamin[emoji120][emoji120]
Hapana wasia kwa warithi (muhammad bin abdillah)
kwa sheria za kiislamu
Sheria ya Islam imeweka sehemu maalumu kwa ajili ya jamaa fulani ya karibu katika mali yanayoachwa na maiti. Mathalan, mke katika hali moja anapokea sehemu ya nne (1/4) ya urithi wa mumewe marehemu na katika hali nyingine apata sehemu ya nane (1/8).

Hiyo ni amri ya Mwenyezi Mungu na mumewe hana haki ya kumwongezea kitu cho chote. Naam, anaweza kufanya wasia wa thuluthi ya mali yake kumpa rafiki zake au jamaa zake wasio na sehemu maalumu katika urithi au mayatima au kwa ajili ya dini. Kwa njia hii M wenyezi Mungu amezuia mtu ye yote asipokee mali nyingi peke yake. Watu wengi wakipata mali kidogo ni bora zaidi kuliko mtu mmoja kupata mali yote. Ndiyo njia ya amani, raha, na starehe.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Amani na upendo vikatawale [emoji1545][emoji1545]
IMG-20191217-WA0000.jpeg
 
Aamin[emoji120][emoji120]
Dunia ndivo konde la Akhera (muhammad bin abdillah)
Kila mtu ni mlimaji na cho chote atakachotenda katika maisha ya dunia mfano wake ni kama mbegu ipandwayo kondeni na yeye atakwenda kuvuna matunda yake baada ya kufa kwake. Basi na aangalie apandacho.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Aamin
Kupeleka rambirambi kuwe mara moja tu (muhammd bin abdillah)
Ni desturi mbaya kukusanyika mahali pa matanga na kukaa hapo hapo siku nyingi kuwatia gharama waliofiwa. Mtu aliyepatwa na msiba lazima apewe mkono wa tanzia maana atafarijika lakini kuiendeleza muda mrefu kutamwongezea huzuni na mzigo.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Amin
Jifunzeni yakin (muhammd bin abdillah)
Yakini maana yake ni kujua jambo fulani kwa hakika kuwa ndivyo. Yakini ndiyo msingi wa matendo yote. Mtu mwenye yakini kuwa mbegu zikipandikizwa zitaota ndiye anayeweza kuzitoa ghalani na kuzifukia ardhini. Watu ambao imani yao inalewalewa hawafiki mahali.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Aamin Mwenyezi Mungu atuongoze kwenye uaminifu[emoji120][emoji120][emoji120][emoji120]
Kuaminiwa ni heshima (muhammd bin abdillah)
Yafaa Mwanadamu akae duniani kwa jinsi itakayompelekea kuaminika. Mtume s.a.w. alipewa lakabu ya ‘Alamin’ (mwaminifu) na watu wake tangu alipokuwa kijana kwa sababu ya maisha yake yaliyotukuka. Mhaini hana heshima.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Amin
Waheshimuni watoto wenu (muhammd bin abdillah)
Mtoto wa leo ni baba wa kesho. Lazima tuwafunze kujiheshimu na hivyo watakuwa na moyo wa kujitoa katika yale yanayowaletea aibu na pia watashika adabu njema ya kuwaheshimu wengine, wakubwa kwa wadogo. Kuwatolea ukali kila mara si vizuri.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom