Winga wa Real Madrid Gareth Bale aliweka mpira wavuni, lakini mwamuzi alikataa bao hilo kwa madai beki wa kushoto wa timu hiyo Ferland Mendy alikuwa katika nafasi ya kuotea.
Matokeo hayo yamezidisha msisimo wa kuwania ubingwa wa Ligi Kuu msimu huu kwa kuwa timu hizo zimeendelea kulingana pointi 36, lakini Barcelona iko kileleni kwa uwiano mzuri wa idadi ya mabao.
Awali, mchezo huo ulipangwa kuchezwa Oktoba 26 kabla ya kuahirishwa kutokana na hali ya kisiasa iliyopo katika Jimbo la Katalunya inapotoka Barcelona wanaotaka kujitenga.
Jambo la kufurahisha licha ya timu hizo kuwa na upinzani mkali, zilikaa hoteli moja na zilisafiri pamoja kwenda uwanjani saa mbili kabla ya mchezo kuanza zikiwa chini ya ulinzi mkali.
Cristiano Ronaldo amefunga bao la aina yake baada ya kuruka kwa umbali wa mita 2.6 kwenda juu katika mchezo ambao Juventus ilishinda mabao 2-1 dhidi ya Samdoria.
Ushindi huo umeiweka kileleni Juventus ‘Kibibi Kizee’ cha Turin katika mchezo msimamo wa Ligi Kuu Italia. Wachambuzi mbalimbali wa soka wamelitaja bao hilo kuwa ni miongoni mwa mabao bora msimu huu.
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.