Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Suarez akwama kufikisha mabao 10

Straika Luis Suarez amefunga mabao tisa dhidi ya Real Madrid kwenye mechi za El Clasico katika La Liga, hivyo aliingia kwenye mechi hiyo akiwa na lengo la kutikisa nyavu kufikisha mabao 10 na pengine kuongezea idadi yake. Suarez ameshindwa kuingia kwenye rekodi ya kuwa mchezaji wa tatu ambao mabao yao yanayoanzia tarakimu mbili nyuma ya Cesar Rodriguez (12) na Lionel Messi mabao 18.
 
Griezmann ashindwa kuwafunga Madrid

Staa mpya wa Barcelona, Antoine Griezmann amefunga mabao saba katika mechi 18 alizocheza dhidi ya Real Madrid kwenye La Liga kwa kuanzia msimu wa 2010/11. Ameshindwa kuwafunga kwenye El Clasico yake ya kwanza, lakini idadi yake ya mabao yanamfanya kuwa wa tatu nyuma ya Lionel Messi (11) na Luis Suarez (9) waliofunga dhidi ya Madrid ndani ya muda huo.
 
Messi afikia rekodi ya Xavi

Katika vitu vitano zilivyokuwa zikisubiriwa kutokea kwenye El Clasico ya Jumatano iliyopita ni kimoja tu kinachomhusu supastaa Messi ndicho kilichotokea, ambapo kitendo cha kuwapo tu uwanjani kwenye mechi hiyo, basi kimemfanya mchezaji huyo kufikia rekodi ya kiungo Xavi Hernandez ya kucheza mechi nyingi za El Clasico. Sasa wawili hao kila mmoja amecheza mechi 42.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…