INATOSHA. Pep Guardiola uvumilivu umemshinda. Ameona sio shida, amechukua uamuzi wa kuwaandikia barua Ligi Kuu England na kuwaambia ‘asante’ baada ya ratiba ngumu iliyopangiwa timu yake ya Manchester City kwenye kipindi hiki cha Krismasi huku wapinzani wake Liverpool akihisi wanapendelewa.
Mabingwa hao watetezi wa Ligi Kuu England wamepewa mapumziko ya mechi kwenye Boxing Day, lakini baada ya hapo watacheza mechi mbili kwa muda usiozidi saa 48.
Kwa kuwalinganisha wapinzani wao kwenye mbio za ubingwa, Liverpool wao wana siku moja zaidi ya mapumziko baina ya mechi zake mbili dhidi ya Leicester City na Wolves.
Guardiola alishasema wakati ratiba inatangazwa kwamba atahitaji kuwaweka kwenye jokofu wachezaji wake kwa siku mbili kutokana na mechi zinazowakabili kwenye Desemba hii.
Kitu pekee ambacho amefanyiwa Guardiola na wachezaji wake ni kwamba wao hawatakuwa na mechi kwenye siku zote za sikukuu, kwa maana ya Krismasi na Boxing Day.

Aliongeza: “Jumapili ni siku ya mapumziko, tutafanya mazoezi Jumatatu na Jumanne asubuhi. Usiku wa Jumanne ni mapumziko, Jumatano asubuhi ni mapumziko, Alhamisi mazoezini na Ijumaa ni mechi dhidi ya Wolves ya Nuno Espirito Santo.”