Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Kkkkkk........
FB_IMG_1577381333465.jpeg


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Manchester United ilicheza mechi 29 bila ya kupoteza kwenye ligi katika awamu mbili tofauti. Kwanza ni kwenye ule msimu waliobeba mataji matatu makubwa, ambapo walianzia Krismasi hadi mwisho wa msimu na mwanzo wa msimu mwingine bila ya kupoteza, hadi walipokuja kufungwa Oktoba 1999, kabla ya kurudia rekodi hiyo kuanzia Aprili 2010 na Februari 2011.
 
Man City – mechi 30

Aprili 8, 2017 hadi Januari 2, 2018

Kikosi hiki cha Manchester City kila mmoja aliamini kwamba huenda kingefikia rekodi ya Arsenal ya kucheza msimu wote kwenye Ligi Kuu England bila ya kupoteza mechi, wakati walipocheza mechi 22 bila ya kupoteza msimu wa 2017/18. Lakini, walikuja kuvurugwa kwa kipigo cha 4-3 kutoka kwa Liverpool, lakini hiyo ilikuwa kabla ya kucheza mechi 30 mfululizo bila ya kupoteza.
 
Liverpool – mechi 34

Januari 12, 2019 – hadi sasa

Liverpool ndiyo timu ya sasa ambayo imecheza mechi nyingi bila ya kupoteza, ambapo tangu Januari 12 mwaka huu, wamecheza mechi 34 hadi sasa bila kupoteza. Wamekuwa na rekodi tamu kwelikweli kwenye Ligi Kuu England ambapo kwa sasa wanaoongoza kwenye msimamo kwa tofauti ya pointi 10. Rekodi yao ya kushinda mfululizo ilivurugwa na Man United msimu huu.
 
Chelsea – mechi 40

Oktoba 16, 2004 hadi Novemba 6, 2005

Wakati Jose Mourinho alipowasili Stamford Bridge mwaka 2004, haraka sana aliibadili timu hiyo na kuwa moto uwanjani, ambapo timu hiyo ikageuka kuwa hatari ndani ya uwanja, ambapo walicheza kwa miezi 12 na wiki tatu bila ya kupoteza mechi yoyote. Rekodi yao hiyo ilikuja kumalizwa na Man United kwenye msimu wa 2005/06, licha ya kwamba Chelsea ilibeba ubingwa.
 
Arsenal – mechi 49

Mei 7, 2003 hadi Oktoba 24, 2004

Wanaoshika namba moja ni Arsenal, hasa kwenye ule msimu wao ambao walicheza bila ya kupoteza mechi kwenye Ligi Kuu England. Arsenal ilicheza mechi 49 bila ya kupoteza. Arsenal walicheza kutoka Mei 7, 2003 hadi Oktoba 24, 2004 bila ya kupoteza mechi yoyote, hadi hapo waliposhindwa kufikisha mechi ya 50, ambapo walichapwa na Man United.
 
Katika msimu wa 2002/03, Henry alipiga pasi za mabao 20 katika msimu mmoja na rekodi hiyo haijavunjwa tangu wakati huo hadi sasa, lakini kwa moto aliyouwasha De Bruyne ni wazi kuwa rekodi hiyo ya gwiji wa Arsenal haiko salama msimu huu.
 
Back
Top Bottom