Mabeki wa pembeni wa Liverpool, Trent Alexander-Arnold na Andy Robertson nao hawako nyuma kwenye mbio hizi za kumsaka mpishi bora wa mabao England, wakati Anorld akiwa amepiga pasi za mwisho sita mwenzake Robertson amefanya hivyo mara tano.
Pacha wa De Bruyne kwenye safu ya kiungo ya Man City, David Silva licha ya kucheza dakika chache kulinganisha na wapinzani wake, ameendelea kukomaa nao akiwa amepiga pasi za mabao saba.
Hatahivyo, vita hii bado haijaisha si ajabu orodha hii kubadilika ifikapo mwisho wa msimu kwa sababu lolote linaweza kutokea kwenye nusu ya pili ya msimu iliyosalia.