Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Wengine wanatamka vinywani kuwa wana malengo ya kufanya vitu kadhaa na yanabaki vichwani na vinywani mwao bila kuyaratibu mahali popote. Wengine wanaandika hayo malengo mahali ambapo watakuwa wanarejea kila wanapotaka kufanya hivyo,katika kipindi chote cha utekelezaji wa hayo malengo.
 
Kinachowaunganisha watu hawa wawili ni kwamba wote wanatamani kutimiza lengo fulani kwa kipindi fulani,ila kinachowatofautisha ni namna utaratibu wao wa maisha. Mmoja mipango na malengo yake yote yako kichwani na mwingine anahamisha kutoka kichwani na kuweka kwenye maandishi.
 
WEKA MALENGO NA KUYAFIKIA KWA MUDA ULIOPANGA

Sasa malengo ni nini?

Mimi huwa nasema malengo ni njia yangu ya maisha.Malengo yangu ni njia yangu ambayo nikiipita itanisaidia kufika kule ninakotaka kufika. Huwezi kufika mahali kama hakuna njia ya kukufikisha huko.
 
Katika maisha lazima uwe na njia ya kuipitia ili ufike kule unakotaka kwenda. Maisha ni kupanga na kupanga ni kuchagua.Unaweza kuamua kupita njia ya jirani yako au kuchonga ya kwako.Unaweza kuamua kupita njia ya mkato au njia ndefu yote ni uamuzi wako.
 
Watu wengi wanachanganya sana kati ya matumaini na maengo wakidhani ni maneno yenye kubeba maana moja. Ila unapaswa kutofautisha kati ya matumaini na malengo.Matumaini ni malengo yaliyokosa mkakati ambayo kila mtu anayo kichwani mwake.Malengo ni matumaini yaliyojengewa mkakati.Huwezi kuishi kwa kutumaini tu hutafika popote na hakuna aliyewahi kufanikiwa kwa kutumaini tu.
 
SOMA MALEMGO YAKO KILA SIKU*

Kuandika malengo na kuyatekeleza ni kitu kizuri lakini kuna nguvu sana kama mtu utakuwa na tabia ya kusoma malengo yako uliyoandika kila siku. Utabaini kuwa kila mara uyasomapo huwa yanakuelekeza njia ya kuipitia na usafiri wa kutumia kuipita hiyo njia kwa siku husika.
 
Utafiti uliofanywa mwaka 2006 na gazeti la U.S.A Today ulibainisha kuwa kuna makundi mawili ya watu walio jiwekea malengo ambao walifanyiwa utafiti.Kundi la watu walioandika malengo yao na wale ambao hawajaandika malengo yao. Mwisho wa mwaka matokeo ya utafiti huo yalionyesha 4% ya wale ambao hawakuandika malengo yao waliweza kufikia malengo yao,lakini miongoni mwao wengine hawakuweza hata kukumbuka walikuwa wamepanga nini!
 
Lakini 44% ya wale waliokua wameandika malengo yao na wengine waliobaki angalau waliweza kukumbuka nini walipanga na kwa nini hawakufanikiwa. Utagundua kuwa katika makundi yote hayo mawili walioandika na wale ambao hawakuandika malengo yao wote wana watu walitimiza na walioshindwa kabisa kutimiza malengo yao. Hata hivyo kwa kuzingatia utafiti huu njia ya kuandika ni ya manufaa zaidi ikilinganishwa na njia ya kutunza malengo kichwani.
 
Hivyo nao walikuwa na kitu cha kujifunza kutokana na kutofanikiwa.Kuandika malengo kunakupa kitu kinachoitwa kitaalam *Psychic neuromotor activity*. Kinakupa akili ya kutilia maanani na kufanya ndani ya akili yako iitwayo *Subconscious mind.*. Sijui mwaka 2019 ulikuwa umejiwekea malengo gani kuyatimiza? Jiwekee nidhamu ya kuandika malengo yako.
 
Kitu kizuri ni kwamba kila mmoja lazima mwisho wa mwaka atimize malengo yake,je unajua anapaswa kutimizaje malengo yako??? Kumbuka usipotimiza malengo yako asili haiwezi kukuacha bila lengo ujue utatimiza malengo ya mtu mwingine.Binadamu hakuumbwa kukaa tu!
 
Back
Top Bottom