Utafiti uliofanywa mwaka 2006 na gazeti la U.S.A Today ulibainisha kuwa kuna makundi mawili ya watu walio jiwekea malengo ambao walifanyiwa utafiti.Kundi la watu walioandika malengo yao na wale ambao hawajaandika malengo yao. Mwisho wa mwaka matokeo ya utafiti huo yalionyesha 4% ya wale ambao hawakuandika malengo yao waliweza kufikia malengo yao,lakini miongoni mwao wengine hawakuweza hata kukumbuka walikuwa wamepanga nini!