Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Kweli tutaona furaha
Tukifika kwenye Raha kuu
Tukisafishwa mioyo yetu
Na Yesu mwokozi

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wanafamilia;

Tayari tumo 2020. Wuhuuu [emoji1734][emoji1734][emoji1734][emoji1734]



Mungu Ametujalia sana na kutupa upendeleo wa ajabu. Tumeuona mwaka mpya (2020). Hebu basi mwaka huu na ukawe wa mibaraka, amani, upendo na utangamano zaidi.

Kwenu bros wote (hasa The King, Kijana Mpole, Ninge, Bradha, Mkokaa na Mfilisti) - love you guys. Bila nyinyi uzi huu utakosa ladha kabisa. Kwa wanaharakati wetu katika uzi huu (hasa Coco na BAK) - endeleeni kupambana mpaka kieleweke na 2020 ndiyo hii.

Kwa Sis wangu wa pekee hapa - dumisha upole na amani yako. Wewe u mfano wa kuigwa. Jirani Yetu Mwema. Endelea kutuombea kwa Molla wetu na kutupa pole bila kuchoka. Wewe ndiye mleta farijiko letu hapa.

Esta. Kusema kweli wewe ndiye injini ya uzi huu. Natumaini 2020 tutaendelea kuwa nawe hapa; na ban zisizo za lazima zitakuepuka. Shemeji yangu kipenzi (aka TRM Kivuruge). Ukiwepo hapa uzi huu huwa unachangamka sana. Najua una majukumu mengi lakini kama anavyosemaga King himuselfu - muda ukipatikana basi tunakutana hapa. Mtazamo wako chanya na posti zako nyingi za kutia moyo huwa zinatubariki wengi. TH mcheshi usiye na makuu. Endelea kuwa nasi. Andaeitini wa Arachuga - busara zako za kiandaeitini na fikra zako komavu pamoja na mitazamo yako chanya bado inahitajika sana katika uzi huu.

Mpendwa wetu Hawachi. Wewe ni mpendwa wa uzi huu na ni mmoja wa watu wanaoheshimiwa sana hapa JF. Japo ulikuwa mkimya ila mwishoni hapa umeweza kufunguka na kuanza kutaniana na kila mmoja japo kwa viwango. Endelea hivyo kwa mwaka huu ili upendwa wako ukaweze kudhihirika zaidi na kutubariki.

Poti unatuhumiwa kuwa umebadilika. Sijui huko ulikokuwa watekaji wamekufanya nini. 2020 tunamtaka poti wetu tuliyemzoea. Poti mbeba maua, magauni ya bluu, viatu vya mchuchumio na makreti ya mvinyo. Tunaomba ucheshi wako urudi. Mishil - moyo wako wa kutokata tamaa na ukaendelee na 2020 hii ikalete utimilifu katika harakati zako zote.

Kwa Wahenga Wenzangu - busara zenu bado zinahitajika sana na mkiona kitu hakijaenda sawa, msikose kutoa mtazamo wenu. Ankoo una uwezo mkubwa wa kiushawishi na zaidi ya mara moja uliwahi kunichomoa kutoka kwenye iginoa listi. Wewe pia ni mwanafalsafa mbobevu na japo huwa unaaandika kidhihaka dhihaka na kiucheshi sana, jumbe zako nyingi huwa zimebeba busara na hekima nyingi ndanimwe. Tunakutegemea sana katika uzi huu kwa mambo mengi.

Kwenu Mashabiki wa Livapuu. Ni wazi mwaka huu ni wenu. Japo ushabiki wenu unakera sana, nawaombea moto wenu usizimike na mwaka huu muweze kutimiza ndoto zenu za muda mrefu na hatimaye muweze kulitwaa kombe la EPL.

Kwenu mliopotea katika uzi huu (na wengine ambao sikuwataja) - Fragaria, Prof, Ledada, Jakitoo, BAK na wengineo, Mungu Awabariki sana huko mliko. Na muda ukipatikana basi msikose kupita hapa kutusalimia.

Binafsi sina kinyongo na mtu hapa na kama kuna mtu ambaye kwa namna moja au nyingine nilimkosea basi naomba msamaha wa dhati. Tuanze mwaka mpya katika upya wake, na kama ambavyo jirani yetu huwa anatukumbusha kila mara, amani na upendo wetu vikadumu. Kwa sasa niko napambana na kijukumu fulani hivi lakini kwa msaada wa Mungu naona karibu kitakamilika; na mambo yakikaa sawa kabisa kwa asilimia mia basi nitarudi tena hapa kwenye uzi wetu kwa ari mpya na nguvu mpya

Blessings and Happy New Year Wanafamilia.

 
Happy New Year Bro SYB

Kurudi kwako ni faraja sana kwetu, Welcome home The Don
 
HAPPY NEW YEAR "LIKES" FAMILY
Hakika hii ni familia kwa hapa Jf heri na baraka tele katika mwaka huu mpya.

Mfanikiwe katika mipango yote mnayoipanga, ukawe mwaka wa kufanikiwa kwa kila mwanafamilia wa "LIKES".

Cheers to a new year and another chance for us to get it right
 
[emoji120][emoji120][emoji120] ahsante SYB. Happy new year
Sent using Jamii Forums mobile app
 
Daah! Asante sana bro..... ubarikiwe sana
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…