Real Madrid bado inataka kumuuza mshambuliaji wa kimataifa wa Wales Gareth Bale, 30, licha ya ajenti wake kutilia shaka uhamisho wake msimu wa joto. (Telegraph)
Spurs wanatafakari uwezekano wa kumsaini mshambuliaji wa zamani wa Celtic Moussa Dembele, 23, kutoka Lyon baada ya kubaini kuwa Harry Kane hatakuwa uwanjani hadi Aprili baada ya kujeruhiwa. (Goal)
Leicester haijakatiza matumaini ya kumsajili beki wa Juventus na Uturuki Merih Demiral, 21, licha ya ofa zao mbili kukataliwa na pamoja na ushindani kutoka Manchester City. (Mirror)
Leicester haijakatiza matumaini ya kumsajili beki wa Juventus na Uturuki Merih Demiral, 21, licha ya ofa zao mbili kukataliwa na pamoja na ushindani kutoka Manchester City. (Mirror)
Mkufunzi wa zamani wa Arsenal Unai Emery amefichua kuwa Everton ilimhoji kwa saa tatu kuhusu usimamizi wa klabu hiyo kabla ya kumuajiri Carlo Ancelotti. (Mail)
Arsenal na Manchester United wamewasilisha ofa ya kumsajili mshambuliaji wa Paris St-Germain na Uruguay Edinson Cavani, 32. (El Chiringuito - via Metro)
Chelsea sasa wanamlenga mlinzi wa West Ham Issa Diop na wanatazamiwa kutuma dau la usajili la pauni milioni 40 kwa Mfaransa huyo mwenye miaka 22. (Express)
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.