Hawakuweza kabisa kuendana na kasi ya washambuliaji wa Manchester City, ambapo hadi kufikia mapumziko tayari walikuwa wameokota mara tatu mipira kwenye nyavu zao, licha ya kwamba bao moja lilikuwa la kujifunga, Andreas Perreira.
Beki ghali, Harry Maguire yupo tayari kucheza akiwa na maumivu ili aitumikie timu kwenye mchezo wao dhidi ya Norwich City, yenye mshambuliaji hatari Teemu Pukki kuweka mambo sawa katika Ligi Kuu England.
Beki Maguire aliyenaswa kwa Pauni 85 milioni kwenye dirisha lililopita la majira ya kiangazi mwaka jana, alipata maumivu ya nyonga kwenye mechi ya sare ya bila kufunga kwenye Kombe la FA dhidi ya Wolves na madaktari walikuwa na hofu huenda angekuwa nje kwa mwezi mmoja.
Hakucheza dhidi ya Man City kwenye Kombe la Ligi wenzake walipochapwa 3-1.
Solskjaer sasa ana kibarua kimoja kinachomkabili, ni suala la kuamua tu kucheza kamari kwa kumtumia mchezaji huyo, kwa sababu kwa kufanya hivyo kunaweza kuongeza ukubwa wa tatizo na kulazimika kufanyiwa upasuaji.
Man United ina mabeki wa kati wawili tu kwa sasa ambao ndio wapo fiti, wote ni majanga, vidumu vya petroli vijana wanasema, kwamba hawakawii kujiripua.