Kutimiza ndoto kuna gharama zake. Kuna muda itakulazimu kuwa macho wakati wengine wamelala. Kuna muda itakulazimu kuachana na baadhi ya tabia unazozipenda. Kuna wakati itakulazimu kuwa mpole hata pale ulipokwazwa, nk. Lakini, gharama zote hizo, ziwe kubwa ziwavyo, haziwezi kufikia gharama za wale ambao hawakuamka kupambania ndoto zao. Kwa sababu, wakati utakapokuwa ukijifuta jasho kwa leso ya hariri huku umepumzika chini ya kivuli cha mafanikio, wao watakuwa wamesimama katikati ya jua kali, wakitafuna mate machungu huku wakijilaumu kwanini walilala.
!
!
!
!
Good morning fam[emoji170]
All the good stuff happens outside our comfort zone.